Daktari Bingwa wa Magonjwa ya mfumo wa mkojo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt Remigius Rugakingira,  ameshauri watu wanaokutwa na UTI mara kwa mara wafanye uchunguzi wa kina kwani wanaweza kuwa na mawe kwenye figo.

Dkt Rugakingira amesema kuna baadhi ya bakteria kwenye mfumo wa mkojo ambao wanafanya utengenezaji wa mawe kuwa mkubwa.

"Mtu anayetibiwaa UTI mara kwa mara anaweza kuwa na bakteria wengi ambao wanatengeza mawe kwenye figo kwa hiyo, ni bora akafanya uchunguzi wa kina" alisema Daktari.

Alifafanua kuwa Hospitali ya Benjamin Mkapa wanaweza kuyabaini mawe hayo kupitia teknolojia ya vipimo ikiwemo CT SCAN na Utrasound na kuwa wanaweza kutibu tatizo hilo pasipo upasuaji kwa kuwa wana mashine ya Shock Wave Lithotripsy (SWL).


SWL ni mashine inayotumia teknolojia kuyeyusha au kuyaponda mawe na kuyatoa kwa njia ya mkojo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...