Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selamani Jafo amesema mazingira ndiyo ajenda inayosababisha uchumi kuwa imara.
Amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi kutoka shule mbalimbali, viongozi na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Februari 7, 2022.
Zoezi hilo ambalo ni miongoni mwa shughuli zinazofanyika kuelekea uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Februari 12, 2022.
Pia, Waziri Dkt. Jafo alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kutumia mvua zinazonyeshja katika maeneo mbalimbali nchini kupanda miti ili ikue na hali itakayosaidia katika kurejesha mazingira katika hali nzuri.
Aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwemo Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wanafunzi na wananchi kwa ujumla kushiriki katika zoezi hilo.
Aidha, waziri huyo alihamasisha wanafunzi hao kupeleka ujumbe kwa wazazi wao kushiriki katika zoezi la kupanda miti katika maeneo yao ili kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga alisema katika zoezi hilo wameweza kupanda ya aina mbalimbali ikiwemo ya matunda na kivuli.
Bi. Maganga alisema kuwa zoezi hilo ni limekwenda vizuri na wamejitokeza kwa wingi kushiriki kupanda miti pamoja na kuwepo kwa changamoto ya kuwepo kwa mvua .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipanda mti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Februari 7, 2022, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Bw. Abdallah Hamis Mitawi akipanda mti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Februari 7, 2022, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipanda mti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Februari 7, 2022, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na wanafunzi kutoka shule mbalimbali na wananchi walioshiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Februari 7, 2022, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021 unaotarajiwa kufanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Februari 12, 2022
Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kati, Dkt. Franklin Rwezamila akipanda mti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Februari 7, 2022, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021.(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Faraja Ngerageza akitoa elimu kuhusu umuhimu wa upandaji miti na uhifadhi wa mazingira kwa ujumla kabla ya kuanza kwa zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Februari 7, 2022, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021.
Meneja Msaidizi wa Maendeleo ya Rasilimali za Misitu kutoka Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Kanda ya Kati, Bi. Patricia Manonga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akipanda mti katika eneo la Medeli jijini Dodoma leo Februari 7, 2022, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...