Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kati) amekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Alfa Care Group Limited Bw. Dadkarim Mulla (wa kwanza kushoto) ambaye aliambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo (wa pili kushoto) walipomtembelea Wizarani tarehe 1 Februari 2022 jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi, katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Edwin Rutageruka (mwenye tai) na Katibu wa Waziri, Bw. Seif Kamtunda.
Katika Mazungumzo yao wamejadili juu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kwa lengo ya kuyafikia malengo ya kitaifa kwa ufanisi.
Vilevile wamejadili namna ya kuongeza uwekezaji katika miradi ya maendeleo husasani sekta ya afya, miundombinu, teknolojia, utalii sambamba na kukuza ajira kwa watanzania.
Mazungumzo yakiendelea.
Picha ya pamoja
Mhe. Balozi Mulamula akimkabidhi Mhe. Gambo Calenda na Shajara za Wizara.
Mhe. Waziri akimkabidhi pia Bw. Mulla calenda ya Wizara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...