MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo la Kipumbwi na Mkwaja wilayani Pangani wakati wa ziara yake ya kuzungumza na kuitambulisha bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo ambao wapo mkoani Tanga na walianzia kwa kutembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine lengo ni kusikia changamoto walizonazo kwenye eneo la kipumbwi na kuona namna ya kuzifanyia kazi kulia ni Ofisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua
Ofisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua akizungumza wakati wa ziara hiyo
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia kushoto akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipumbwi wakati wa ziara yake
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia aliyevaa shuti nyeusi akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkwaja Mhekezi Mwinyi Pembe wakati wa ziara yao
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia wa pili kutoka kushoto akitembelea maeneo mbalimbali mara baada ya kufika eneo la Kijiji cha Mkwaja wakati wa ziara yake

NA OSCAR ASSENGA, PANGANI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia ametoa wito kwa wavuvi na wasafirishaji Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani Mkoani Tanga kuacha kutumia vyombo vya kubebea mizigo kwa ajili ya kusafiria badala yake watumie vile vilivyoruhusiwa kisheria.

Hatua hiyo inatokana na eneo la Kipumbwi kushamiri vitendo vya abiria na mizigo kupanda kwenye vyombo vya kusafirishia mizigo kufanya safari zao kati ya Kipumbwi kuelekea Visiwa vya Unguja na Pemba na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha yao na mali.

Captain Mandia aliyasema hayo wakati wa ziara kuitambulisha bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo ambao wapo mkoani Tanga ambapo walianzia kwa kutembelea Bandari ya Tanga na maeneo mengine lengo ni kusikia changamoto walizonazo kwenye eneo la kipumbwi na kuona namna ya kuzifanyia kazi

Alisema kwao Kama Shirika wanasimamia ulinzi na usalama wa usafiri majini hivyo Serikali itachukua njia nzuri za usafiri bila kupoteza maisha na mali zenu hivyo alihaidia kulichukua suala hilo na kuhakikisha linafanyiwa kazi.

“Sisi kama Shirika jukumu letu ni kusimamia ulinzi na usalama niwahaidi suala la chombo cha usafiri hapa Kipumbwi tunalichukua na kuona namna linafanyiwa kazi”Alisema

“Hata leo asubuhi wakati nazungumza na Mkuu wa wilaya ya Pangani nimemueleza tutakachofanya kwa mamlaka tulionayo ni kuangalia namna ya kuboresha sheria, kanuni na taratibu tulizonazo kufikia mahali ambapo kutakuwa na vyombo vizuri kwa ajili ya kusafisha watu”Alisema Captain Mandia

Hata hivyo aliwaambie wananchi wa eneo hilo kwamba chao kimefika serikali na watalifanyia kazi ili kuona namna ya kulipatia ufumbuzi kwa lengo la kuondosha changamoto iliyopo.

Akizungumzia suala la Light House kwenye eneo hilo,Captain Mandia alisema kwamba wao Shirika wanajukumu la kudhibiti vyombo vya usafiri hivyo watawaelekeza Bandari kwamba kila wanaporasimisha wajitahidi kuhakikisha kuweka vitu ambavyo vinahitajika ili kuwasaidia wananchi ikiwemo kuweka (Light Huose) Taa,

Alisema taa hizo ambazo zitakuwa zikiwaka zitakuwa zikiashiria eneo husika ili kuweza kuwaepusha kupotea wanapokuwa majini wakiendelea na shughuli za uvuvi.

Kuhusu chombo cha uokoaji alisema tayari wao Tasac wanakuja na utaratibu huo na inategemea na bajeti maana nchi inasehemu kubwa sana ya maji hivyo wamelichukua na kuona namna ya kulifanyia kazi.

“Lakini kitu ambacho mngeweza kukifanya wavuvi na wasafirishaji mizigo wapeni elimu lugha ya kuwasiliana bahati nzuri wana simu za mikononi zinatumia satelite kwa hiyo wachukue kuna frequare ambazo wanatumia namba za simu wanazotumia kwa hapa wawasiliane na Bandari ya Tanga na Pengine Pangani ni rahisi mtu kusema tupo eneo Fulani tunahitaji msaada ili kuweza kuwasaidia kuwaokoa wanapopata majanga baharini”Alisema Captain Mandia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...