Na Jane Edward, Arusha
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI)Tengeru imeanza uzalishaji wa aina mpya za mbegu bora Chotara za migomba zinazoweza kuzaa kwa muda mfupi na kinzani kwa magonjwa ya mnyauko.
Akizungumza wakati wa ziara ya kimafunzo kwa waandishi wa Habari na watafiti Kaimu Meneja TARI Tengeru Fatma Hussein iliyoandaliwa na Serikali chini ya Tume ya Taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH).
Ambapo amesema mbegu hizo aina za Matooke ambazo zimepewa majina ya TARIBAN1, TARIBAN2, TARIBAN3,TARIBAN4 zitaongeza uzalishaji na kipato kwa wakulima nchini.
"Kati ya sifa zilizopo kwenye aina hizi za ndizi ni kutumika kama chakula, Juice na Bia na wakulima wananufaika nazo kwa kujiingizia kipato"Alisema Fatma
Nao baadhi ya wakulima wanaonufaika na mbegu hizo Mathayo Abraham Akyoo anasema mbegu za zamani zilikuwa zikishambuliwa na magonjwa na uzalishaji wake ulikuwa ni mdogo ambapo mbegu hizi za sasa uzalishaji wake ni mkubwa.
Aidha wameeleza kuwa soko la ndizi hizo ni zuri na kwa sasa wanapata kipato cha kujikimu kimaisha tofauti na hapo awali.
Teknolojia hiyo ya mbegu zinazo zalishwa katika Taasisi ya utafiti wa kilimo -TARI Tengeru imepata ufadhili wa Serikali kupitia COSTECH ambapo wamekarabati na kutengeneza maabara nne na vifaa ambazo zinawawezesha kuzalisha mbegu kwa kiasi kikubwa kwa njia za kimaabara.
Kazi ya kuikagua Mbegu za migomba ikiendelea.Baadhi ya watafiti wakiandaa migomba kwaajili ya kupelekwa kwa wakulima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...