Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kampuni tanzu inayotoa huduma za mawasiliano kwa nchi 14 ukanda wa bara la Africa, leo wametangaza habari njema kwa wateja wake wote nchini wanaotumia huduma za vifurushi vya muda wa maongezi (bando za muda wa maongezi) kwa kuongeza dakika za bando kwa zaidi ya mara 2 pamoja na muda wake wa kutumika gharama ikiwa ni ileile.
Tumebusti bando zaidi ya mara mbili, bando ya Tsh 500 ilikuwa unapata dk 40 lakini kuanzia sasa, leo hii kwa Tsh 500 ilele unapata dakika 100 tena zikiwa zimeongezwa na muda wa kuzitumia ili kumfanya mteja afurahie thamani ya fedha yake zaidi.
Kwa wale wanaotumia Bando ya Tsh 1000 Tumebusti kwa kuongezea muda wake wa kutumia sasa itadumu kwa siku 2 ikiwa na dakika zaidi na gharama yake ni ilele, kwa bando za Wiki na Mwezi tumezibusti kwa kuziongezea dakika zaidi ili kuwafaidisha zaidi wateja wanaonunua bando kwa Wiki au Mwezi
Bando mpya za dakika za muda maongezi sasa zitakuwa kama ifuatavyo:
Bando hizi zimetengenezwa kwa kuzingatia sana mahitaji na matumizi ya wateja wetu, tumezingatia sana thamani na ubora huku gharama ikiwa nafuu zaidi. TumeBusti itasaidia sana wateja kuweza kuendelea kupanga vyema mpango wa matumizi kwa kufaidika na muda tuliiongezea kwenye bando hizo pamoja kulingana na uhitaji au matumizi.
Ili kufaidika na TumeBusti, Kupata dakika mara 2 kwa vifurushi vya muda wa maongezi mteja atatakiwa kupiga *149*99# na kujiunga na kifurushi kinachomfaa. Pia mteja anaweza kujinunulia kifurushi kupitia huduma ya Airtel Money kwa kupiga *150*60# na kuchagua Nunua Bandona unafuu ni uleule ukiwa popote.
Airtel Tanzania inaendelea na dhamira yake ya kutoa huduma za mawasiliano ya bando nafuu huku pia ikiendelea na uwekezaji kwenye mtandao wa kasi kwa masafa Interneti ya Airtel SUPA 4G ambapo tayari imeshaeneza mitambo hiyo nchini kwa zaidi ya asilimia 60 ili kuwapa watumiaji wa Smartphone nchini Tanzania huduma ya haraka na uhakika wakiwa popote.
Akiongea haya kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Bw, Dinesh Balsingh Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Airtel Bi, Beatrice Singano alisema:
Mkurugenzi Mawasiliano Beatrice Singano (kulia) na Meneja Uhusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando wakionesha bango baada ya Airtel kutangaza habari njema kwa wateja wake wote nchini wanaotumia huduma za vifurushi vya muda wa maongezi (bando za muda wa maongezi) kwa kuongeza dakika za bando kwa zaidi ya mara 2 pamoja na muda wake wa kutumika gharama ikiwa ni ileile.Mkurugenzi Mawasiliano Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari wakati kutangaza habari njema kwa wateja wake wote nchini wanaotumia huduma za vifurushi vya muda wa maongezi (bando za muda wa maongezi) kwa kuongeza dakika za bando kwa zaidi ya mara 2 pamoja na muda wake wa kutumika gharama ikiwa ni ileile. Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...