Mwamvua Mwinyi,Pwani
WATU
wawili wamefariki dunia pamoja na kujeruhi wengine wawili ,katika ajali
iliyohusisha magari matatu kugongana huko maeneo ya Miwaleni,
Halmashauri ya wilaya Kibaha Vijijini mkoani Pwani.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa polisi Mkoani Pwani,Pius Lutumo alieleza, ajali hiyo imetokea march 28 asubuhi.
Alieleza
kuwa, gari namba T608 AGV likiwa na tela lenye namba T.317 AQM aina ya
scania likiendeshwa na Raymond Kimaro (36) ,mkazi wa Ubungo likitokea
nchini Kongo kwenda Dar es salaam ambapo lilihamia upande wake wa
barabara na kugonga gari namba T.256 CMF aina ya Noah iliyokuwa ikitokea
Dar es Salaam kwenda Morogoro.
Alieleza,hali
hiyo ilisababisha kontena kuchomoka na kuangukia gari SU 38223 aina ya
Toyota land cruiser iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kwenda Morogoro
ikiendeshwa na Innocent Gerson Mringo na kusababisha vifo na majeruhi
hao.
Lutumo alitaja
waliofariki dunia kuwa ni profesa Prosper Ngowi (55) mhadhiri wa Chuo
Kikuu cha Mzumbe, Na Innocent Gerson (33) mkazi wa Dar es Salaam na
dereva.
Majeruhi ni
Raymond Kimaro (39) dereva wa lori T.608 AGV na Abdallah Mohammed
(33)dereva wa Noah mkazi wa Dar es Salaam na kusababisha uharibifu wa
magari.
Kamanda huyo
alifafanua, chanzo Cha ajali bado kinachunguzwa hata hivyo uchunguzi wa
awali unaonyesha Kuwa ni uzembe wa dereva wa gari aina ya scania kuhama
upande wake wa barabara na kugonga gari aina ya Noah na kupelekea
kontena kuchomoka na kuliangukia gari Toyota cruiser.
Lutumo
alisema, mwili wa marehemu profesa Prosper Ngowi umehifadhiwa hospital
ya rufaa Tumbi na mwili wa marehemu Innocent Gerson umehifadhiwa katika
kituo cha afya Mlandizi.
Majeruhi wametibiwa na hali zao ni nzuri huku mtuhumiwa akishikiliwa na jeshi la polisi kwa hatua zaidi.
Lutumo aliwaasa madereva kuacha kuendesha pasipo kufuata Sheria za Usalama Barabarani,na wawe makini ili kujiepusha na ajali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...