Na Humphrey Shao, Michuzi Tv.

 CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimesema asilimia 60 ya wahitimu wake wanajiajiri na kuajiri wengine hivyo kimeamua kujikita kwenye mafunzo ya vitendo ili kutatua tatizo la ajira.

 Hayo yalisemwa jana na Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho, (Taaluma, Utafiti na Ushauri), Profesa Edda Lwoga, wakati wa mkutano na Mameneja Rasilimali Watu (HROs) na Masoko kutoka makampuni mbalimbali.

 Alisema mkutano huo unalenga kupata mrejesho wa utendaji kazi wa vijana wanaohitumu kwenye chuo hicho na kujiweka sawa ili kutoa elimu inayoendana na elimu ya biashara kwenye soko la ajira.

Alisema mwaka 2016 chuo hicho kilifanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 60 ya wahitimu wake wamekuwa wakijiajiri na na kuajiri wenzao na ndiyo sababu wakaamua kujikita kwenye mafunzo ya vitendo.

“Tulifanya utafiti kwa kuwafuatilia wahitimu waliomaliza kwenye chuo chetu na kubaini kwamba asilimia 60 wamejiajiri na kuajiri wenzao na tulipata matokeo yaliyosababisha tufanye maboresho kwenye mitaala yetu,” alisema

Aidha, alisema kwa sas wamekuja na mafunzo ya vitendo ambapo mwanafunzi kwenye program yake anakuwa darasani kwa nusu na muda mwingine anakuwa kwa mwajiri.

  Alisema wameamua kufanya hivyo ili kumoa ujuzi mwanafunzi ili hatimaye aweze kuajiriwa au kujiajiri mwenyewe pindi anapomaliza masomo badala ya kuhangaika kutafuta ajira ambazo ni chache sana.

“Pia tumeanzisha utaratibu ambapo mwanafunzi mwenye wazo la biashara anakuja nalo tunamtafutia mwalimu wa kumfundisha ili aweze kuanzisha kampuni yake na kufanya biashara na kuajiri wengine anapomaliza masomo yake hapa,” alisema

 Naibu Mkuu wa chuo hicho, (Mipango na Fedha), Dk. Emmanuel Munishi, alisema kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya elimu ya biashara, chuo kimepanga kujipanua kwenda Zanzibar, Lindi na Iringa

 “Tumewaita nyie kwasababu ndio mnaamua watu wafanyekazi kwenu au la kwasababu nyinyi ndio mnahusika na kuajiri sisi kazi yetu ni kufundisha, nyinyi ni wadau muhimu sana kwa kuwa mnatengeneza mipango ya kuajiri,” alisema

  “Tumewaita muangalie namna tunavyowaandaa hawa wafanyakazi wenu watarajiwa na sehemu ambazo tunatumia kuwaandaa mtushauri namna bora ya kuendelea mbele, tunataka mtushauri kwasababu inawezekana bado tuna mtazamno wa zamani tuambieni tuendeje,” alisema

Alisema program za CBE zimebadilika sana na wamefanikiwa kufanya maboresho makubwa kwenye miaka ya karibuni kutokana na mahitaji ya soko kubadilika.

 Alisema chuo hicho kimeanzisha program zaidi ya 26 na kwamba miaka mine iliyopita walianza kufundisha Sahada mbili za Uzamili lakini mpaka mwaka huu zimefikia 10.

 “Tunatoa kozi za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na Masoko kwajili ya kuleta wataalamu wenu kuja kuongeza elimu tumefundisha wataalamu wetu na sasa walimu 32 wamesoma mpaka kiwango cha PhD,” alisema

Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho, (Taaluma, Utafiti na Ushauri), Profesa Edda Lwoga, akizungumza na  Mameneja Rasilimali Watu (HROs) na Masoko kutoka makampuni mbalimbali.
Naibu Mkuu wa chuo hicho, (Mipango na Fedha), Dk. Emmanuel Munishi, akizungumza na Maofisa Rasilimali watu ambao walifika katika chai Maalum iliyoandaliwa na chuo hicho kwa ajili ya maofisa hao
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...