Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

KAMATI ya siasa Kibaha Mjini kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani, Ramadhani Maneno imeridhishwa na ujenzi wa mradi wa barabara kwa kiwango cha lami TAMCO Vikawe-MAPINGA km. 23 unaotarajiwa kugharimu zaidi ya sh. Bilioni 35,hatua inayokwenda kuunganisha wilaya za mkoa huo na kuinua uchumi.

Aidha kamati hiyo ,imepitia pia mradi wa ujenzi wa barabara Pichandege (Sheli) hadi hospital ya wilaya ya Lulanzi utakaogharimu sh.milioni 500 kutoka mfuko wa Jimbo Kibaha Mjini.

Mwenyekiti wa CCM Pwani,Maneno alisema , barabara hizo Ni muhimu kwani itafungua milango ya kimaendeleo na zitakomboa wananchi waliokuwa wanapata kero ya vumbi kutokana na miundombinu isiyo rafiki.

Alisema kuwa, Serikali imejipanga kuboresha miundombinu mbalimbali ya barabara kwa viwango mbalimbali kulingana na mahitaji ya eneo husika na kiwango cha bajeti iliyopangwa.

"Kazi yetu Chama Cha Mapinduzi ni kusimamia utekelezaji wa ilani,kwani miradi hii tunakwenda kuisemea kwa wananchi na kuhakikisha inaleta tija kwao kimaendeleo"alieleza Maneno.

Nae Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini,Maulid Bundala alitaka kuona taarifa ya kwenye karatasi iwe ya uhakika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kama walivyoieleza.

"Nashukuru pia Mwenyekiti wa CCM mkoa kuamua kuja kuungana na sisi , kamati ya siasa mkoa imejigawa katika wilaya mbalimbali na yeye akaamua kuja Kibaha Mjini ,tunamshukuru "alisema Bundala.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara TAMCO Vikawe -MAPINGA mwakilishi kutoka Wakala wa barabara (TANROADS Pwani, Evelyn Mlai alieleza, Wakala huo inasimamia matengenezo na ujenzi wa barabara hiyo urefu wa km.23.

Evelyn alifafanua,kati ya kilometa 23 kilometa 2.9 zimemalizika eneo la Machinjioni na Pangani, wakandarasi wanaendelea na ujenzi kwenye km 5.1 ambapo km 14.94 zilizobaki ziko hatua ya manunuzi.

Awali mwakilishi kutoka Wakala wa barabara Vijijini (TARURA ),Bupe Angetile alisema, ujenzi wa barabara Pichandege Sheli hadi hospital ya wilaya Lulanzi ina jumla ya km.2.67 itakamilika Mei mwaka huu.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Mshamu Munde alieleza, miradi ya kimkakati inaendelezwa na hasa kuboresha miundombinu ya barabara na sekta ya afya ili taswira ya mji iendelee kuonekana.

Alisema Mradi wa barabara Pichandege- Sheli hadi hospital ya wilaya Lulanzi inajengwa kiwango cha lami mita 550.

Kamati hiyo pia imekagua mradi wa kuweka transfoma tatu na kujenga msongo wa kati maeneo ya Mpiji-Muheza na mradi wa kati kutoka Luguruni hadi TAMCO kwa kutumia nguzo za zege.

Miradi mingine iliyopitiwa ni ,kituo cha afya Kidimu na kukagua mradi wa tenki maji maji Vikawe kata ya Pangani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...