Na.Khadija Seif Michuzi

BARAZA la Sanaa Taifa (BASATA) limeingilia kati Mgogoro wa ndani  la Shirikisho la Muziki na kusimamisha uteuzi wa awali wa Msemaji wa Shirikisho hilo Steven Mengere .

Aidha Baraza limetoa uamuzi huo mara baada ya kufanya kikao Machi 23 na kuridhia kuwa Msemaji huyo kutoanza Majukumu yake Hadi pale sakata hilo litakapotatuliwa.

Pia Baraza limejiridhisha kuwa Bodi ya utendaji ya Shirikisho lilifanya kikao chake mapema Machi 1 katika ukumbi wa Bodi ya Filamu na kufanya uteuzi huo.

Baraza limetoa taarifa ya kushughulikia Mgogoro huo na kupokea hoja za wajumbe pamoja na viongozi wa Shirikisho hilo na na kuahidi kutoa uamuzi mapema iwezekanavyo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...