BENKI ya Exim Tanzania na Jumuiya ya Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI) wametiliana saini Mkataba wa Makubaliano (MoU) ya ushirikiano wa kiutendaji hatua inayolenga kuinua kuboresha utoaji wa kwa sekta ya utalii katika Visiwa hivyo vya kihistoria.

Ushirikiano huo unatoa wasaa kwa wadau hao wawili kushirikiana katika kuhakikisha taarifa zote muhimu kuhusu utalii visiwani humo Zanzibar zinapatikana kwa urahisi duniani kote na kuhakikisha kwamba wanachama wa ZATI wanapata ufumbuzi wa mahitaji yao yote ya huduma za kifedha.

Akizungumza wakati hafla fupi ya utiaji saini makubaliano hayo iliyofanyika Zanzibar mwishoni mwa wiki Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Bw Simai Mohamed pamoja na kuwapongeza wadau hao wawili kwa hatua hiyo alitayataja makubaliano hayo kuwa ni ya aina ya kipekee yakiwa yameainisha viashiria mahususi vya utendaji kwa pande zote mbili ili kuwezesha maendeleo ya miundombinu bora ya utalii na shughuli kote Visiwani.

Alisema hatua hiyo inakwenda sambamba na azma ya serikali ya kuimarisha ushirikiano miongoni mwa taasisi za sekta binafsi pamoja mahusiano baina ya serikali na sekta binafsi.

“Ni imani yangu kuwa mahusiano mazuri baina ya wadau wa serikali na taasisi za kifedha ikiwemo benki ya Exim yatasaidia zaidi wadau mbalimbali wa utalii Zanzibar ambao wameathiriwa kwa kiasi kikubwa na athari za kiuchumi za COVID-19 ili waweze kujikwamua na hatimaye kurejesha uwezo wao wa kiuchumi. Natoa wito kwa taasisi nyingine za fedha kuiga mfano huu kwa kuwa karibu na wadau wa utalii hasa katika zama hizi ambapo serikali inajikita zaidi katika uchumi wa bluu ‘’ alisema.

Utalii unachangia takribani 25 asilimia ya pato la Taifa Zanzibar (GDP) na hadi asilimia 80 ya mapato ya fedha za kigeni visiwani humo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu alisisitiza kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo kuendelea kukuza sekta ya Utalii Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

"Sekta hii muhimu ya utalii ni moja ya sehemu ambayo tunaitazama zaidi hususani katika visiwa hivi vya Zanzibar na maeneo mengine hapa nchini hivyo na niahidi kwamba tutaendelea kujidhatiti zaidi hilo. Utalii ni nguzo muhimu ya uchumi wa Zanzibar na sisi tutaendelea kuzingatia hilo kwa kuwekeza zaidi muda wetu, juhudi , rasilimali watu na mtaji zaidi katika kuhudumia sekta hii na msimamo wetu huo hautabadilika’’ alisisitiza.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo ya miaka mitatu, benki hiyo itahusika katika kuhakikisha wadau wa utalii wanapata mikopo ya biashara kubwa na ndogo inayoandaliwa kulingana na mtiririko wa fedha za mwanachama husika.

“Pia tutaendelea kutoa huduma bora zaidi za kubadilishia fedha kwa kuzingatia viwango vyenye ushindani zaidi kwa sarafu zote ikiwemo Shilingi ya Kitanzania pamoja na Dola ya Kimarekani.

Ni kutokana na mkakati wetu huu ndio maana hata kwenye matawi yetu tunahakikisha kwamba wadau wa utalii hususani wanachana wa ZATI wanakuwa na upendeleo maalum katika kupata huduma, ikiwemo kupatiwa Meneja Mahusiano maalum kwa ajili yao tu.

Pia tunahakikisha wanapata huduma nyingine nyingi ikiwemo huduma za Bima, uwepo wa makubaliano maalum katika viwango vya ushuru (tarrifs) pamoja na kuwapatia Mashine za malipo (POS) ili kuwarahisishia watalii kufanya malipo na kutokuwa na wasiwasi wa kubeba au kutembea na pesa.’’ Alisema Matundu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ZATI, Rahim Bhaloo, aliipongeza Benki ya Exim kwa ushirikiano huo, na kusema hatua hiyo itaiwezesha sekta ya kimkakati ya utalii Zanzibar kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wake, kuinua ubora wa huduma na kuongeza zaidi mvuto wa Visiwa hivyo kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.

“Ni muhimu kueleza kuwa hatua hii ni matokeo ya ushirikiano wa karibu na wenye tija kati ya ZATI na wadau wake wakiwemo wanachama wake, taasisi za fedha kama Benki ya Exim na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ushirikiano huu huu utatuwezesha kusaidia ipasavyo biashara yetu ya utalii, kutengeneza ajira, na kuboresha ustawi wa wawekezaji wadogo na wakubwa katika sekta ya utalii.’’ Alisema.



Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (kushoto) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI) Bw. Rahim Bhaloo (kulia) wakitia saini hati za Makubaliano ya kiutendaji baina ya taasisi hizo mbili mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki. Ushirikiano huo unatoa wasaa kwa wadau hao wawili kushirikiana katika kuhakikisha taarifa zote muhimu kuhusu utalii visiwani humo zinapatikana kwa urahisi duniani kote na kuhakikisha kwamba wanachama wa ZATI wanapata ufumbuzi wa mahitaji yao yote ya huduma za kifedha. Wanaotazama ni Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed (katikati), Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaaban (wa pili kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Fatma Mabrouk (wa tatu kulia) na wawakilishi wengine kutoka sehemu zote mbili.




Ushirikiano huo unatoa wasaa kwa wadau hao wawili kushirikiana katika kuhakikisha taarifa zote muhimu kuhusu utalii visiwani humo Zanzibar zinapatikana kwa urahisi duniani kote na kuhakikisha kwamba wanachama wa ZATI wanapata ufumbuzi wa mahitaji yao yote ya huduma za kifedha.




Akizungumza wakati hafla hiyo Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Bw Simai Mohamed (Pichani) pamoja na kuwapongeza wadau hao wawili kwa hatua hiyo alitayataja makubaliano hayo kuwa ni ya aina ya kipekee yakiwa yameainisha viashiria mahususi vya utendaji kwa pande zote mbili ili kuwezesha maendeleo ya miundombinu bora ya utalii na shughuli kote Visiwani.


Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaaban akizungumza kwenye hafla hiyo.




Akizungumza kwenye hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (Pichani) alisisitiza kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa mkakati wa benki hiyo kuendelea kukuza sekta ya Utalii Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.



Akizungumza kwenye hafla hiyo Mwenyekiti wa ZATI, Rahim Bhaloo (Pichani) aliipongeza Benki ya Exim kwa ushirikiano huo, na kusema hatua hiyo itaiwezesha sekta ya kimkakati ya utalii Zanzibar kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wake, kuinua ubora wa huduma na kuongeza zaidi mvuto wa Visiwa hivyo kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.



Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed (Katikati walioketi), Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaaban ( wa tano kulia walioketi) na Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Fatma Mabrouk (wa pili kulia walioketi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na maofisa wa Benki ya Exim pamoja na Jumuiya ya Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI) wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya Makubaliano ya kiutendaji baina ya taasisi hizo mbili mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...