Mkurugenzi wa Rasilimali watu na huduma wa Mamlaka
ya Usafiri wa Anga Tanzania ( TCAA), Teophory Mbilinyi akizungumza kwa
niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo wakati wa hafla ya
kuwatunuku vyeti wahitimu wa Mafunzo ya Uongozaji Ndege kwa kutumia
rada, Ufundi wa Mkanda wa kupokea Mizigo katika Viwanja vya ndege pamoja
na Usalama katika Viwanja vya ndege yanayotolewa na Chuo cha Usafiri
wa Anga Tanzania (CATC).
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ambaye ni Mgeni Rasmi, Bw. Hamisi Amiri akizungumza
wakati wa hafla ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa Mafunzo ya Uongozaji
Ndege kwa kutumia rada, Ufundi wa Mkanda wa kupokea Mizigo katika
Viwanja vya ndege pamoja na Usalama katika Viwanja vya ndege
yanayotolewa na Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC).
Baadhi ya wahitimu wa kozi ya Uongozaji Ndege kwa kutumia rada wakifuatilia hotuba katika mahafali chuoni hapo.
Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC), John Ndimbo
akizungumzia namna walivyoendesha mafunzo hayo kwa ufanisi na kwa
kuzingatia ubora kimataifa.
Mtaalam
wa Uundaji wa mitaala na mafunzo kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri
wa Anga Duniani (ICAO) Bw. Simon Lugaba akielezea hatua walizopitia
katika kuusuka mtaala ambao licha ya kwamba utatumika kufundisha
wataalam utauzwa kwa vyuo vingine na kuingizia kipato CATC.
Wahitimu wakifuatilia yanayoendelea
Kwa
niaba ya wahitimu wote Bw. Godlove Longole ambaye ni muongozaji ndege
muandamizi akiushukuru Uongozi wa Chuo kwa namna ilivyoaandaa na
kuwasilisha mafunzo hayo kwao.
Picha za pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...