Na Mwandishi Wetu

ChemChem Maji Moto ya Utete, Rufiji yaendelea kuwa kivutio kwa watalii kutoka pande mbali mbali.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya kutembelea kivutio hicho, Mhifadhi Misitu wa Wakala Wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Shafiu Hamza Rajab amesema kuwa wamejipanga kuendelea kupokea wageni wengi zaidi ili kufika kujionea maajabu ya mwenyezi Mungu.

Amesema kuwa chem chem hiyo inafaida kubwa kwa wakazi wa Rufiji kwa vile maji hayo hutumika katika masuala ya mila na kunywa kwa vile ni salama.

Maji hayo ambayo yanachemka nyuzi 90, yamepimwa na mkemia mkuu na kugundulika ni salama kwa matumizi ya binadamu.

Vile vile amesema kuwa wakazi wa Utete wamekuwa wakiyatumia maji hayo katika kutoa mikosi na magonjwa ya ngozi.

Ameongeza kuwa wakala wa Huduma wa Misitu wamezidi kusimamia vyema, ambapo mwaka 2009 walipokabidhiwa Chemchem hiyo walikuta joto la nyuzi 45 ila kwasasa limepanda kufika nyuzi 90 kutokana na utunzaji mzuri.

Jambo lingine la kuvutia amesema kumekuwa na majani ya ajabu yaitwayo ndango ambayo huota sehemu za joto lakini eneo hilo linabaridi na yamestawi.

Ametoa wito kwa Watanzania kwenda kuona maajabu ya mwenyezi Mungu katika kivutio hicho ambacho ni adimu maeneo mengine.



ChemChem Maji Moto ya Utete, Rufiji
Mhifadhi Misitu wa Wakala Wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Shafiu Rajab


Watalii wakifurahia madhari ya ChemChem Maji Moto ya Utete, Rufiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...