*Kaizen yawa mpango mzima kubadili fikra ya utendaji

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

 Wadau wa Usafirishaji wa Mabasi yaendayo kasi (DART) wapewa mafunzo ya utendaji kazi wa Kaizen kuendana na kasi katika utoaji wa huduma ya usafirishaji kwa jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART)kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji ,Deus Kasmir amesema wadau wa usafirishaji wakijua falsafa ya Kaizen kutakuwa hakuna muda wa kupoteza na matokeo yake kama taasisi itakuwa na mafanikio yanayoendana na utoaji wa huduma bora.

Amesema kuwa mafunzo hayo ni ya awamu ya pili ambapo kila mtu katika nafasi yake ameshirikishwa katika kuendana na falsafa ya Kaizen kufanya kuimarisha mifumo ya utoaji huduma zinazokwenda na viwango vyake.

Kasmir amesema nchi zilizotekeleza Falsafa ya Kaizen kwa Taasisi na Kampuni ya Biashara zimepiga hatua ambapo hata Tanzania tunakwenda kwa kasi na DART ndio sehemu ya kutumia falsafa hiyo ikiwa ni kuimarisha mifumo ya utendaji ya kuharakisha huduma zilizo bora.

Amesema kazi ya kutoa huduma kwa wananchi ndio msingi wa maendeleo ya nchi hivyo ni vyema kila mmoja kusimama katika kutenda kazi.

Aidha amesema changamoto ambazo ziko katika sekta hiyo ni fursa za kuendana na kupata utatuzi wenye kuimarisha sekta ya usafirishaji.

Nae Mhadhiri wa Chuo cha Biashara (CBE) Dk.Mariam Tambwe amesema kuwa katika biashara kuna mambo mengi kama sehemu ya kutoa elimu lazima kila mtu ajue nafasi yake.

Kwa upande wake Mhandisi wa Uendeshaji wa DART na Mratibu Katondo Nambiza amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwani yanajenga kuimarisha huduma.

Mkurugenzi wa Fedha na Maendeleo ya Biashara wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Deus Kasmir  akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadau wa usafirishaji wa DART katika kuendana na Falsafa Kaizen ,jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa Uendeshaji wa DART na Mratibu wa Kaizen  Katondo  Nambiza akizungumza kuhusiana na mafunzo ya Kaizen katika uboreshaji wa huduma kwa wateja wenye matokeo ,jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Chuo cha Biashara (CBE) Mariam Tambwe akizungumza kuhusiana na umhimu wa mafunzo yatayosaidia kutoa huduma bora ,jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na wadau wa usafirishaji DART mara baada ya kufunguliwa kwa mafunzo ,jijini Dar es Salaam.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...