Kutokana
na mgao wa maji uliokuwepo kwa wakazi wa Chalinze, Mamlaka ya Majisafi
na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) sasa imehitimisha
changamoto hiyo ya muda mrefu ya maji.
Akizungumza
wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa maji wa Mlandizi -
Chalinze - Mboga Mwenyekiti wa Bodi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange
amesema kuwa wakati umefika kwa wakazi wa Chalinze na maeneo ya karibu
kupata majisafi kwani mradi huo umekamilika hivyo amewataka wananchi
kwenda kwenye ofisi za Mamlaka hiyo ili kuweza kujisajili kwa ajili ya
kupatiwa huduma ya maji ili kutimiza lengo la Rais Samia la kumtua Mama
ndoo kichwani.
"Leo
nimekuja na wajumbe wa Bodi ili kujihakikishia kama kweli zile fedha
tunazozihidhinisha kama kweli zinahakisi kilichopo kwenye miradi husika"
alisema Mwamunyange
Pia
Mwamunyange amesema Bodi imefuatilia na kukagua uchimbaji, ulazaji wa
Bomba pamoja na ujengaji wa Pampu za kusukumia maji na wamejiridhisha
mradi huo umekamilika kwa asilimia mia hivyo imebaki kazi ya wananchi
kuanza kutumia maji ya mradi huo.
Naye
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Mradi wa Maji wa Ruvu
Juu hadi Mboga ni Mradi unaenda kuondoa kero ya upatikanaji wa Maji
katika maeneo ya Mlandizi, Chalinze na Mji Mdogo wa Mboga, pia Mradi huu
umelaza mabomba ya inchi 12 kwa umbali wa Kilomita 59 kutoka mtambo ya
Ruvu Juu hadi Chalinze, Mji wa Mboga.
Pia
amesema kiasi cha Shilingi Bilioni 18 kimetumika kwenye Miradi wa Maji
wa Ruvu Juu mpaka Msoga itakayotatua kero ya Maji kwa wananchi zaidi ya
122,000 wa maeneo hayo hivyo kumalizika kwake itakuwa ndio suluhu la
upatikanaji wa maji kwenye mji wa Chalinze, Pingo, Pera, Msoga,
Bwilingu, Msata, Kihangaiko, na Ubenazimozi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar
es Salaam (DAWASA), Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akipata maelezo
kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu
toleo(Off take)ya kutoa maji kutoka Mtamboni kwenda kwenye mradi wakati
wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa
Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na Chalinze awamu ya lll.
Bodi
ya Wakurugenzi wa DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali
Mstaafu Davis Mwamunyange wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA)
Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mtambo wa kusukumia maji wa Ruvu Juu
wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ya kukagua mradi wa
maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na Chalinze awamu ya lll.
Bodi
ya Wakurugenzi wa DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali
Mstaafu Davis Mwamunyange wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA)
Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze -
Mboga uliogharimu takribani bilioni 18 pamoja uendeshaji wa pampu ya
kusukumia maji ya Chamakweza wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa
DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na
Chalinze awamu ya lll.
Bodi
ya Wakurugenzi wa DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali
Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi
na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja
wakimsikiliza Meneja wa DAWASA Chalinze Mhandisi Pascal Fumbuka
alipokuwa anatoa taarifa ya wateja ambao wameweza kufungiwa huduma ya
maji katika eneo la Chamakweza wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa
DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na
Chalinze awamu ya lll.
Muonekano wa Pampu ya kusukumia maji ya Mboga
Bodi
ya Wakurugenzi wa DAWASA ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali
Mstaafu Davis Mwamunyange wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA)
Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu Pampu ya kusukumia maji ya Mboga
wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA ya kukagua mradi wa
maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na Chalinze awamu ya lll.
Ziara ikiendelea
Mwenyekiti
wa Bodi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam
(DAWASA) Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza na waandishi wa
habari mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa
DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na
Chalinze awamu ya lll.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa Mlandizi Chalinze-Mboga
uliogharimu sh. Bilioni 18 na kulaza Bomba kubwa za inchi 12 kwa
Kilometa 59 mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa
DAWASA ya kukagua mradi wa maji wa Mlandizi-Chalinze - Mboga pamoja na
Chalinze awamu ya lll.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...