Na Jane Edward, Arusha

Mkuu wa wilaya ya Arumeru mhandisi Richard Ruyango amezindua zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji cha chemchem ya Moivaro iliyopo katika kitongoji cha Moivaro kijiji cha Shangarai kata ya Ambureni lengo likiwa ni kufanya chanzo hicho kuwa endelevu.

Akizindua zoezi hilo mhandisi Ruyango alisema kuwa miti waliyoipanda ikawe ishara ya kukikafanya chanzo hicho kiendelee kuwa na maji lakini pia amewataka wananchi wanaolima mboga aina ya Saladi katika chanzo hicho kuziondoa na hadi ifikapo march 26 saa nane mchana zoezi hilo liwe limekamiluka huku waliojenga ndani ya chanzo kubomoa nyumba hizo ndani ya mwezi mmoja.

Ruyango amesema baadhi ya watu wamekuwa wakiharibu vyanzo vya maji jambo ambalo halikubaliki hivyo wote wanaofanya shughuli za kibinadamu katika chanzo hicho waondoe kwa muda uliyowekwa kwani baada ya hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kufikishwa mahakamani.

“Kwa mwaka 2021 halmashauri ya Meru tumepanda miti 1600 na kwa mwaka huu wa 2022 tumeshapanda miti 725 ambapo lengo letu ni kufikia miti milioni 1.5 lakini pia natoa rai kila mtoto apewe mti mmoja wa matunda aupande pamoja na kutunza na hii itasaidia kuja kuwa na kizazi kitakachokuwa rafiki wa mazingira,” Alisema Mhandisi Ruyango

Kwa upande a wake Mhandisi wa mazingira kutoka bonde la Pangani Malegeri Joseph akitoa taarifa ya chanzo alisema kuwa maji yanayotoka eneo hilo yanatumika katika matumizi mbalimbali lakini kumekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo watu kufanya shughuli za kilimo ndani ya chanzo, ujenzi, ukataji miti pamoja na uchepushaji wa maji bila kufuata taratibu.

Naye Kaimu mkurugenzi wa bonde la Pangani Godwin Kapama Alieleza kuwa kampeni hiyo ya upandaji miti ni endelevu na litaendelea hadi msimu wa mvua utakapoisha ambapo wanalengo la kupanda miti zaidi ya laki moja katika vyanzo mbalimbali vya maji vilivyopo ndani ya bonde la Pangani.

Alisema kuwa chanzo hicho kumekuwa na changamoto nyingi ambazo wamekuwa wakipambana nazo kwa muda mrefu ambapo wameona katika zoezi hilo la upandaji miti ni muhimu wakaanza na eneo hilo ili waweze kukihifadhi vizuri.

Naye diwani wa kata ya Ambureni Faraja Maliaki alisema kuwa wamepokea maagizo ya mkuu wa wilaya na watayatekeleza ambapo wataanza zoezi la kuondoka mboga zilizopandwa ndani ya chanzo pamoja na kutunza miti ambapo amewataka wananchi kila mmoja kuona kuwa ni wajibu wa kila mmoja kutunza chanzo hicho lakini pia mazingira.

Kaimu Mkurugenzi wa bonde la Pangani Godwin Kapama akiongea na waandishi wa habari baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti
Mkuu wa wilaya ya Arumeru mhandisi Richard Ruyango akiongea na wananchi mara baada ya kuzindua zoezi la upandaji miti katika chanzo cha maji cha Moivaro
Mkuu wa wilaya Arumeru akisalimiana na wanafunzi wa Moivaro.
Hapa Mkuu wa wilaya Arumeru akipanda mti kuashiria zoezi la utunzaji mazingira.
Wakinyanyua mikono kuashiria uzinduzi wa zoezi la upandaji miti.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...