SERIKALI ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imewataka vijana kupitia mradi Youth Agency Mufindi (YAM) kuunda vikundi vya kiuchumi ili kunufaika na mikopo isiyo na riba toka Halmashauri badala ya kukaa Vijiweni bila kazi .

Rai hiyo ilitolewa jana na mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule wakati akizungumza na vijana 100 wanaotoka kwenye mazingira magumu kata za Ihanu ,Luhunga na Mdabulo wanaoendelea na mafunzo ya Afya ya akili kwenye Ukumbi wa Yatima Igoda .

Mtambule aliwataka vijana hao kuunda vikundi na wale wenye ulemavu kuungana hata wawili ama mmoja kuomba mkopo .
Alisema serikali ya wilaya haitapenda kuona vijana wakizurula mtaani ama kushinda Vijiweni bila kazi na kuwa watakaokamatwa watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili wafungwe gerezani wakafundishwe kufanya kazi huko.

Akielezea Kuhusu mafunzo hayo aliwataka vijana waliobahatika kuzingatia masomo hayo na kutokukatishwa tamaa na changamoto wanazokumbana nazo bali wajipe moyo na kuamini kuwa wakati wao wa kuinuka ni sasa hivyo hawana budi kukabiliana na changamoto hizo.

Aidha aliwataka kutumia fursa hiyo ya mafunzo vizuri kwani serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hasan imejipanga vyema kuwainua na kuwasaidia wahitaji wote kutokana na kutenga fedha nyingi katika Halmashauri zao hivyo wanachotakiwa kufanya ni kujitambua .


Aliongeza kuwa baada ya kupata mafunzo hayo jambo la msingi ni kuyatekeleza kwani utekelezaji wao utapunguza mazingira ya vitendo vya uhalifu na ukatili wa kijinsia katika jamii zao huku akiwataka kuwatumia viongozi wao wakati wanapohitaji msaada

Wakizungumzia baada ya mafunzo hayo wanufaika hao walisema wamejipanga vyema katika kuyapokea mafunzo kwani wanaamini ndoto zao za muda mrefu zitatimia lakini pia wataweza kumudu maisha yao pamoja na kuzikabili changamoto za maisha kwa ujumla.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Dkt. Heriel Mfangavo alisema mafunzo hayo yamejikita katika kuwasaidia vijana namna ya kujitegemea katika nyanja zote ili waweze kujikwamua katika changamoto wanazozipitia lakini pia kujiinua kiuchumi kwa kufanya shuguli mbalimbali za ujasiriamali .


Dkt Mfangavo aliongeza kuwa vijana ambao wanastahili kukaa kwenye makundi baada ya mafunzo hayo wananufaika kwa kupata mikopo kutoka katika bajeti za halmashauri ambayo itawasaidia katika kuendeleza biashara zao lakini pia vijana ambao ni walemavu wanapewa kipaumbele cha kuweza kukopeshwa au kuingizwa kwenye fursa za ajira rasmi .

Meneja wa mradi wa YAM Zilpa Mgeni alisema mradi huo unaendeshwa Kwa ushirikiano na serikali na hivyo wanaishukuru serikali kwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na mradi wao ambao kiujumla una msaada mkubwa sana kwa vijana .

''Mimi na timu yangu tumeona huu mradi unasaidia kwasababu tumegundua kuwa kuna mbadaliko makubwa tangu tumeanza kuwabainikwani hapo mwanzo walikuwa hawajiaamini kwamba wanaweza kufanya biasharalakini baada ya kupata mafunzo ya saikolojia na ujasiriamali wao wenyewe wamekiri kwamba wanaweza kufanya kitu ''. alisema Zilpa

Pia aliiomba serikali kuzidi kutoa ushirikiano hasa kwa kusaidia kupatikana kwa mikopo hiyo ili wanufaika hao wapate mitaji na kuweza kujiendeleza kimaendeleo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi na diwani wa kata ya Luhunga Festo Mgina aliwataka vijana hao kusikiliza vyema mafunzo hayo huku akiwaahidi kuwa pamoja na kuwahakikishia kupata mikopo baada ya mafunzo yao kutokana na serikali kujipanga vyema katika kuwasaidia wahitaji.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...