*Wakili wa GSM adai kuwa mwenye vielelezo zaidi hivyo awasilishe 

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Sakata la Kiwanja No.60 kilichopo mtaa wa Regent Estate eneo la Mikocheni  kati ya Ghalib Said Mohamed na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa zamani Paul Makonda limechukua sura mpya baada ya Ghalib Said Mohamed kuomba huruma kwa waandishi kuwa ni mali yake kwa vielelezo vya umiliki wa kiwanja hicho.

Katika kiwanja hicho hivi karibuni kulibuka kurushiana risasi na kuwaondoa walinzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kile kinachoitwa mafundi na walinzi walikuwa sehemu isiyo na umiliki wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Sakata hilo limefanya Ghalib Said Mohamed kumtuma Wakili wake Alex Mgongolwa kuzungumza na waandishi  wa habari leo kunabaisha kwa vielelezo juu ya uhalali wa kiwanja hicho kuwa ni Ghalib Said Mohamed.

Amesema mauzino ya kiwanja hicho yalifanyika mwaka 2012 wakati huo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam.

Mgongolwa ameshusha nondo zote zinazomfanya mteja wake GSM kuwa na uhalali na kuonyesha kuwa hata ujenzi huo ulifanyika kwa kuonyesha GSM  kwa kibali chake ni mwaka 2016.

Aidha amedai kiwanja hicho kimenunuliwa kwa Shilingi milioni 640 na zikionesha mauzino kutoka mtu mwenye kiwanja kwenda kwa GSM.

Amesema mahusiano ya GSM na Makonda hakufanyi kuhalalisha kiwanja kilichonunuliwa na GSM kuwa ni mali ya Makonda na kutaka Makonda kuwasilisha vielelezo vya kisheria vikionesha ni mali kiwanja na ujenzi ni mali yake pamoja mashahidi.

Amesema kuwa kuna upotoshaji katika jambo hilo kazi waliopewa ni kuhakikisha wanalinda nembo ya biashara ya Jina la GSM ndani na nje.

Amesema kuwa mtu anadiwa kupora kiwanja na ujenzi wake Paul Makonda anatkiwa kufuata sheria ikiwemo kwenda mahakamani.

Aidha amesema miliki ya ardhi inataratibu zake ambazo GSM amezifuata juu ya umiliki wa kiwanja pamoja na ujenzi  wake kwa mkandarasi kulipwa na huyo mteja wake.

Mgongolwa amesema kufahamiana sio tija kinachotakiwa ni ushahidi wa vielelezo ambavyo kama yeye alivyoonyesha kwa mteja wake huyo.

Mwanasheria wa Gharib Said Mohamed(GSM) ,Wakili Alex Mgongolwa  akieleza namna mteja wake anavyomiliki kiwanja hicho.
Mwanasheria wa Gharib Said Mohamed(GSM) ,Wakili Alex Mgongolwa akiwaomba Waandishi wa Habari wamsaidie kueleza ukweli juu ya umiliki wa kiwanaj No 60 Kilichopo Ligent Estate Mikocheni
Baadhi ya Nyaraka alizokuja nazo wakili wa GSM Katika Mkutano wake na waandishi wa habari


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...