*Yaelezwa wasiokuwa na elimu ya fedha ni wagumu katika kufanya maamuzi
Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV.
Vijana
na Wanafunzi wa Shule za Sekondari pamoja na Msingi wametakiwa
kujengwa katika masuala ya fedha ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi kwa
kujiletea maendeleo.
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Chama cha
Wahasibu Wanawake (TAWCO ) Tumaini Lawrence wakati wa maadhimisho ya
Wiki Fedha Duniani ambayo imeratibiwa na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)
Kampas ya Dar es Salaam ,amesema kuwa suala la fedha linatakiwa kila
mmoja ajue kwani asilimia 54 ya watu wanaopata msongo wa mawazo ni
kutokana na fedha.
Amesema wiki ya Fedha Duniani tangu kuanza
kuadhimishwa lengo lake lilikuwa ni watu kupewa uelewa wa fedha kwani
wakijengwa wanakuwa watu makini na hata wakiwa kazini hawawezi kuwa wala
rushwa.
"Watu kuwa na uelewa wa fedha katika kufanya mipango
tangu akiwa na umri mdogo ni vigumu katika umri mkubwa kuweza kupangilia
fedha kwani ndio anakuwa amezipata kwa mara ya kwanza hivyo lazima
jamii ielemishwe masuala ya fedha "amesema Tumaini
Tumaini
amesema Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Tawi la Dar es Salaam wameona
mbalimbali katika kushirikisha wanafunzi wa Vyuo , Shule za
Sekondari,Msingi pamoja na wadau wa Kilimo na Mifugo kwa kuamini kuwa
ndio watu kupata elimu hiyo katika kujijenga kifikra katika masuala ya
Fedha.
Mratibu wa Wiki ya Fedha wa IAA Vaileth Maira amesema
katika wiki hiyo itakuwa yenye mafakio ya kuwajenge a uwezo wadau pamoja
na kuwa na mjadala wa masuala ya fedha.
Mkuu wa Idara ya Uhasibu na Fedha (IAA) Kampas ya Dar es Salaam CPA Faiza Msheri akizungumza kuhusiana na umhimu wa wiki ya fedha iliyofanyika katika hicho jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Wiki ya Fedha Duniani wa IAA CPA Vaileth Maira akizungumza kuhusiana na wiki hiyo na umhimu wadau kupewa elimu ya masuala ya Fedha jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi pamoja na meza ya mgeni rasmi wakionesha vipeperushi vya Wiki ya Fedha Duniani katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampas ya Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi na waandaji wa Wiki ya Fedha Duniani wakiwa nyuma yq mgeni rasmi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...