Adeladius Makwega-DODOMA


Kama nilivyoeleza katika matini iliyotangulia namna nilivyomfahamu Mike Mhagama ambaye alikuwa DJS wa awali na aliyewahi kuucheza muziki wa kizazi kipya wakati huo akiwa na Redio One & ITV.

Leo hii naendelea na ndugu huyu ambaye hivi sasa yupo Marekani.

Mhagama alisema kuwa kuwa wakati huo Joseph Haule na wenzake walikuwa wakipatikana katika Mtaa wa Ali Khan upo Upanga Jijini Dar es Salaam na nyuma ya mtaa huo walikuwapo jamaa zake hivyo alipokuwa akipita alikuwa akiwakuta ndugu hawa na akizungumza nao.

“Walirekodi album yao ya awali kabisa iliyokuwa inafahamika kama Funga Kazi, mwaka 1993 nadhani album hii haikuwa katika kiwango kinachotakiwa lakini hatimaye mwaka 1994 walitoa album yao nyingine maarufu kama Mambo ya Mjini, album hii ndiyo iliwatambulisha rasmi katika ulimwengu wa Hip Hop ya Tanzania na wakawa miongoni mwa makundi yaliyokaribia kushika hatamu za muziki huo hapo Tanzania wakati huo.”

Kulikuwa na makundi mengi ya muziki huolakini Hard Blasterz walikuwa ni kundi tatanishi kwa makundi mengine kama KWANZA UNITY, DIPLOMATS, DAR YOUNG MOB, WAGUMU HALISI, GANG STARS with MATATIZO.

Nilipokuwa nikifahamiana nao kwa mara ya kwanza niligundua jambo la tofauti kabisa kwa Joseph Haule.

“Huyu alikuwa akifahamika kama Kijana Msogo(kijana mpenda kusoma) ambaye alikuwa akipenda shule sana sana tofauti na vijana wengine walivyokuwa na hili lilikuwa tofauti na mitazamo ya wengi.”

Hapa Mike Mhagama alikwenda mbali zaidi ya watu wengi wanavyomfahamu Profesa Jay huku akitoa sifa ya ukimya na upole.


“Hata katika mahojiano yaliyokuwa yakifanywa dhidi ya muziki huo, Terry Msiaga na Wiliam Shundi wao ndiyo walikuwa wazungumzaji wakubwa huku yeye akiwa kimya sana.”

Profesa Jay aliendelea na muziki wake na sasa aliamua kuwa mwanamuzi binafsi. Kuanzia mwaka 2000 na jambo hilo lilimpeleka mbali sana kisanaa na baadaye kuingia katika siasa hadi kuwa mbunge wa Mikumi.

Profesa Jay na Sugu walionesha njia kuwa Hip Hop haikuwa uhuni bali ilikuwa inaonesha hadharani matatizo ya jamii ambayo yalihitaji kutatuliwa.

Mike Mhagama anamuombea heri Profesa Jay apone haraka ili aweze kuendelea na maisha yake vizuri.

Mwanakwetu huyo ndiyo Joseph Haule kama alivyofahamiana na Mike Mhagama miongoni mwa MadJ wa awali kabisa walioucheza muziki huo kati ya 1990- 2000 akiwa na Redio One na ITV


Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...