Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
KAMATI
ya Bunge ya kudumu ya Nishati na Madini, imeiagiza Wakala wa Nishati
Vijijini (REA ) pamoja na Wizara ya Nishati kuongeza usimamizi kwenye
miradi ya REA Mkoani Pwani na nchi nzima kijumla ili ikamilike kwa
wakati, ifikapo Desemba mwaka huu.
Aidha
imeeleza, Serikali inaendelea kuhakikisha umeme unafika Vijijini na
maeneo ya pembezoni ili kuinua uchumi na maendeleo katika maeneo hayo.
Wakitembelea
baadhi ya miradi ya REA awamu ya III mzunguko wa pili, wilayani
Mkuranga Mkoani Pwani, wajumbe wa kamati ya Nishati na madini
,iliyoambatana na timu ya REA, TANESCO na Wizara ya Nishati, wilayani
Mkuranga Mkoani Pwani, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dustan Kitandula
aliwataka wakandarasi wote nchini kukamilisha miradi hiyo kulingana na
mkataba.
Alieleza, mradi wa REA awamu ya III mzunguko pili ulianza agost mwaka 2021 na unatakiwa kukamilika Desemba mwaka huu.
"Tumekuja
kufuatilia utekelezaji wa miradi tuliyoipitishia fedha mwaka uliopita
kwa wilaya ya Mkuranga,tulipitisha Bilioni 8.1 kwa ajili ya Vijijini 43"
"Mkandarasi
amejitahidi,Ila changamoto muda uliobaki Ni miezi Tisa ,muda huo ni
mfupi,hatuna Shaka Kama miradi hataisha kwa wakati Lakini usimamizi na
ufuatiliaji Ukilegalega tutajikuta wakandarasi wanaomba muda wa
nyongeza"alifafanua Kitandula.
Kwa
upande wake Waziri wa Nishati, January Makamba alisema wamepokea
maelekezo na Nia ya Wizara na Serikali ni kuona mradi unanufaisha
wananchi lengwa.
Makamba
alisema, Serikali inatenga fedha nyingi na Rais Samia Suluhu Hassan
amejipanga kufikisha umeme Vijijini na kuona matokeo ya chanya katika
miradi inayopelekewa fedha .
Alielekeza,shule
ya Makele kata ya Njianne ifikishiwe umeme ndani ya wiki mbili ili
walimu na wanafunzi waweze kufanya majukumu yao ya kielimu vizuri.
Awali
Mkurugenzi REA, Mhandisi Hassan Saidy akitoa taarifa ya utekelezaji wa
miradi ya usambazaji wa umeme awamu ya III mzunguko wa pili, alisema
vijiji 333 kati ya 442 vimepatiwa umeme kupitia miradi mbalimbali sawa
na asilimia 75.
Vitongoji
vilivyopatiwa umeme ni 1,050 kati ya 2,028 ambayo ni asilimia 52,
vijiji 109 kati ya 442 sawa na asilimia 25 bado havijaunganishiwa.
Saidy
alisema vijiji 89 kati ya 109 ambavyo bado havijaunganishiwa umeme
vitapatiwa umeme katika mradi wa REA awamu ya III mzunguko wa pili ambao
upo hatua ya utekelezaji.
Anaeleza
mkandarasi China Railway CRCEBG anaendelea na utekelezaji wa mradi,na
aliongeza mradi huo kupeleka umeme vijiji 89 visivyo na umeme utagharimu
sh.Bilioni 37.4.
Michael
Ngonyani kutoka Mercados Aries (mkandarasi),alisema watahakikisha
wanatekeleza mradi kwa wakati licha ya changamoto wanazokabiliana nazo.
Ngonyani
alieleza wanakabiliwa na changamoto ya Ununuzi wa vifaa gharama kupanda
,vifaa vinavyopatikana nje ya nchi kutofika kwa wakati wakati wa Covid
19 pia upatikanaji wa nguzo kuchelewa.
Diwani
kata ya Njianne Ally Mbwera na mkazi wa Njianne ,mzee Omary Ally
walishukuru Serikali kwa kufikisha umeme Vijijini hususan vijiji vya
kata hiyo ikiwemo Ming'ombe na Makele.
Waliomba usambazaji uongezwe maeneo yaliyobakia na Taasisi za umma na Taasisi za kidini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...