Janeth Raphael - MichuziTv
Serikali Imesema imefanikiwa katika udhibiti wa dawa za kulevya ikiwemo kukamata jumla ya kilo 35, 227.5 ambazo zilijumuissha kilo 1124.52 za heroini gram 811.3 za Cocaine , kilo 22,741.10 za bangi, kilo 10,931.72 za Mirungi, gram 4.92 za Morphine na kilo 428.60 za Methamphetamine
Hayo yamezungumzwa leo 9 Machi, 2022 Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na vyombo vya habari kuhusu mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais @samia_suluhu_hassan
Balozi Chana amesema jumla ya vijana 200 wanaopatiwa matibabu kwenye kliniki zae Methadone wamejumuishwa katika program ya kukuza ujuzi kupitia vyuo vya VETA ili kuwajengeea ujuzi wa kufanya kazi za kiuchumi na kuachana na dawa za kulevya.
Balozi Chana amesema katika mwaka huo mmoja wa Rais Samia jumla ya kliniki sita (6) za tiba ya Methadone zimeanzishwa ambapo kliniki moja (1) ipo mkoani Songwe katika mji wa Tunduma, kliniki zingine nne (4) zipo Jijini Dar es salaam katika maeneo ya Tegeta, Segerea, Mbagala na Kigamboni na kiwango Cha unyanyapaa kimeshuka kutoka asilimia 28 mwaka 2013 hadi asilimia 5.5 mwaka 2021.
Uanzishwaji wa kliniki hizo kunafanya jumla ya Kliniki 15 kuwepo nchini zikihudumia zaidi ya waathirika 10,600 wa dawa za Kulevya kila siku.
"Katika kipindi cha mwaka Mmoja tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani tumeshuhudia Serikali ikiendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi kubwa. Vilevile, huduma kwa wananchi zimeendelea kuboreshwa kwa kiwango kikubwa ambacho sisi sote hapa ni mashahidi" Amesema Balozi Chana
Kuhusiana swala la ugonjwa wa UKIMWI Waziri Pina Chana amesema Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kudhibiti athari za Virusi vya UKIMWI na UKIMWI nchini kwa kutelekeza programu mbalimbali za utoaji elimu na huduma kwa wananchi.
"Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja mafanikio ya Serikali yaliyoshuhudiwa katika eneo hili ni: -
a) Kushuka kwa kiwango cha unyanyapaa katika jamii kutoka asilimia 28 mwaka 2013 hadi asilimia 5.5 mwaka 2021. Mafanikio haya ni kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.
b) Kupungua kwa vifo vitokanavyo na UKIMWI kwa asilimia 50 ambapo vifo vimepungua kutoka 64,000 mwaka 2010 hadi 32,000 mwaka 2021.
c) Kupungua kwa kiwango cha maambukizi mapya ya VVU kwenye jamii ikiwemo maambukizi mapya kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto kushuka kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asilimia 7 mwaka 2021.
d) Pia, Tanzania ipo kwenye hatua nzuri za kufikia malengo ya Kidunia ya Tisini Tatu (90-90-90-) mwaka 2020 na Tisini na Tano Tatu (95-95-95) mwaka 2025. Hadi sasa WAVIU wanaofahamu hali zao za mambukizi ni asilimia 83, WAVIU wanaofahamu hali zao za mambukizi na wapo kwenye matibabu ni asilimia 98 na WAVIU waliopo kwenye matibabu na wamefubaza VVU ni asilimia 92.
Aidha Balozi Chana amesema Baada ya Serikali kufanya maamuzi makubwa ya kuhamia Dodoma kwa lengo la kufanya Serikali kuwa katikati ya nchi na kuwa karibu na Mikoa yote nchini ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi, Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuratibu utekelezaji wa maamuzi hayo kama ifuatavyo yafuatavyo: -
a) Uzinduzi wa ujenzi wa majengo ya Ofisi za Wizara na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mji wa Serikali-Mtumba ulifanyika Desemba, 2021.
Ujenzi wa Ofisi hizo unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwaka 2022/23. Majengo ya Ofisi hizo yatakapokamilika yatatosheleza mahitaji ya wafanyakazi wa Wizara zote.
b) Ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara zenye urefu wa KM 51.2 katika mji huo zinajengwa kwa kiwango cha lami.
"Tunaishukuru Serikali kwani katika mwaka 2021/22 jumla ya Shilingi bilioni 300 ziliidhinishwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi na Miundombinu katika Mji wa Serikali Mtumba" Amesema Balozi Chana.
Hata hivyo Balozi Chana amesema Serikali katika kipindi cha mwaka mmoja imeendelea kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi ya ukuaji wa demokrasia nchini ikiwemo kuwezesha ushiriki wa wadau wote katika kujadili masuala la demokrasia nchini.
Waziri Balozi Chana pia alitembelea ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma leo Machi 9, 2022.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...