Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

MRADI Mkubwa wa ujenzi wa kituo cha kupozea umeme Luguruni-Tamco Kibaha upo kwenye hatua ya ujenzi kwa zaidi ya asilimia 90,na unatarajiwa kukamilika mwezi wa nne mwaka huu ambapo utagharimu Bilioni 15.2 .

Kukamilika kwa ujenzi huo ni sehemu ya kupunguza ama kuondoa changamoto ya kukatika katika kwa umeme suala ambalo wananchi wengi wamekuwa wakililalamikia .

Msimamizi wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha kupozea umeme Luguruni-Tamco Kibaha ,Mhandisi Dickson Usimuogope alieleza ,Lengo la Shirika la Umeme TANESCO pamoja na Serikali ni kuondokana na kero ya kukosa umeme wa uhakika nchini na Viwandani.

Alibainisha ,ujenzi huo una transfoma mbili kubwa ,zenye MVA90 kila moja ,mradi umepata fedha za ndani ya Shirika na Serikali ambapo ukikamilika utasaidia kupeleka umeme mkoa wa Dar es Salaam na Pwani .

Usimuogope alisema ,itakuwa na Faida ya kuimarisha na kuboresha upatikanaji wa umeme ,kwani kitakuwa na matoleo ama fida sita ya msongo wa kilovolt 33 .

Alisema matoleo mawili yataenda Kibaha Mkoani Pwani ambapo moja
Kati yake limeelekezwa eneo la Viwanda TAMCO na jingine litalisha kwa wananchi wa Mailmoja.

"Toleo jingine litakuwa kwa ajili ya hospital ya Mloganzila -MUHAS kutokana na umuhimu wake ,pia Kisarawe,Visiga na toleo la sita Ni Mbezi."Tupo hatua nzuri, asilimia Zaidi ya 90, na tunatarajia April 30 kukabidhi "

Usiogope alifafanua, kutakuwa na uwezo wa transfoma hizi kusaidiana ,endapo umeme ukikatika Mkoani Pwani Basi Dar inapokea hapo hapo bila umeme kukatika,pamoja na Hilo kuna nyaya zimelazwa chini ya ardhi ambazo radi ikipiga inasambaa chini ya ardhi na haiwezi kuathiri transfoma hizo.

Maulid Bundala ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kibaha Mjini ,alifika kutembelea mradi huo akiwa ameambatana na kamati ya siasa wilaya na baadhi Mkoa , alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kukabiliana na kero ya upungufu wa Nishati ya umeme nchini .

Bundala alieleza kwamba, 2024 -2025 suala la kukatika kwa umeme linaweza kuwa historia ,na wanatarajia CCM kujivunia na Kuwa na la kusema kwenye utekelezaji mzuri wa ilani upande wa Umeme Vijijini na pembezoni mwa miji .

Mwenyekiti wa CCM Pwani, Ramadhani Maneno alisema ,kituo hicho wameridhika na ujenzi unavyoendelea.

 



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...