Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kuwepo kwa ushindani wa soko la ajira kitaifa na Kikanda ni fursa muhimu katika kuongeza kasi ya kuimarisha sekta ya elimu nchini.
Mhe. Othman ameyasema hayo leo akiwa katika muendelezo wa ziara yake katika sekta ya elimu kuona changamoto na jitihada zinazofanywa na serikali na sekta binafsi kuendeleza sekta hiyo hapa Zanzibar.
Mhe. Othman amesema hivi sasa dunia inaendelea kubadilika na kusisitiza kwamba sekta ya elimu kwa kuwa ndio sekta mama, Zanzibar nayo ni lazima kwenda sambamba na mabadiliko hayo katika kuzingatia mahitaji ya soko kwa kuandaa na kuzalisha wataalamu wenye kuhumili ushindani wa ndani na nje ya nchi.
Aidha Mhe. Othman amesema ni muhimu kufanya mapitio katika maeneo mbali mbali ya elimu ili kujipanga vyema kwa kuzingatia haja ya wataalamu wenye uwezo mkubwa unaohitaji katika Kanda ya Afrika Mashariki na kwengineko duniani.
Pia emeshauri kwamba kuna haja na umuhimu mkubwa kwa vyuo kubuni na kuendeleza programu mbali mbali zinazohitajika katika soko la ndani na nje na kuchangia kwa kasi kubwa maendeleo ya nchi.
Amefahamisha kwamba kwa kuwa kunawepo mahitaji makubwa na tofauti ya kielimu kwenye maeneo na kada mbali mbali kuhitajika pia kuwepo mipango sahihi kwa serikali ikishirikiana na sekta binafsi katika kuendeleza vyema sekta hiyo ya elimu nchini.
Aidha amesema kwamba changamoto kubwa iliyopo pia ni kwa serikali kujipanga katika mazingira ya sasa kwenye sekta ya elimu kwa kuwepo mipango na mfumo bora utakaokidhi mahitaji kwa kwa mazingira ya sasa na ya baadaye.
Naye waziri wa Elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Leila Mohammed Mussa , ameuagiza uongozi wa Chuo cha Kiislamu kujitathimini ikiwa ni pamoja na kubuni mipango na programu zenye manasaba na mahitaji ya elimu nchini.
Naye Mwalimu Mkuu wa Skuli ya FEZA Mwalimu Ali Nungu, amesema kwamba changamoto kubwa inayopo katika sekta ya elimu Zanzibar ni wataalamu wenye uwezo mkubwa kutoridhia kufanya kazi ya uwalimu kutokana na kuwepo maslahi madogo
Amesema kwa vile elimu ni chimboko la wataalamu wa aina zote ni lazima sekta hiyo kuaangaliwa zaidi kutengenezwa mazingira kuvutia zaidi vijana wenye sifa na uwezo wa kufundisha kujiunga na kada ya ualimu kuliko ilivyo sasa kwamba wengi wanaojiunga huwa ni chaguo baada ya kukosa kwenye vipaumbele vyao vya awali katika kada nyengine za taaluma.
Katika ziara hiyo Mhe. Othman leo ametembele Skuli ya Laurant Chukwani, Chuo cha Kiislamu Mazizini na Skuli ya Fedha Kisauni kuangalia changamoto na jitihada mbali mbali zinazoendelea katika sekta ya elimu nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...