Imeelezwa kuwa mabadiliko ya tabia Nchi athari yake ni kubwa sana hasa katika mfumo wa chakula
Hayo ameyazungumza leo jijinie Dodoma na Mkurugenzi wa Idara ya usalama wa chakula Wizara ya Kilimo Dkt Honest Kessy katika mkutano wa Kitaifa wa matokeo ya tafiti zilizofanywa na mradi wa AFRIKAP ambao ulikuwa ukitekelezwa na taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF) katika Mkoa wa Tanga Wilaya za Lushoto na Muheza
Dkt Kessy amesema mifumo ya chakula ni pamoja na swala la uzalishaji hadi kufikia mlaji wa mwisho
"Katika utafiti huu matokeo ambayo tumeyapata yatatueleza sisi kama Serikali ni mikakati gani tuweke au namna gani ya kuweka mikakati ambayo tutaitengeneza ili sasa tuweze kukabiliana na haya mabadiliko ya tabia Nchi na jamii yetu ya Watanzania isiweze kuadhirika kutokana na mabadiliko haya" - Amesema Dkt Kessy.
Aidha Dkt Kessy amesema utafiti huo ni muhimu sana mana utaipatia Serikali kielelezo katika kuandaa Sera na mikakati mbalimbali kama Serikali.
Hata hivyo Dkt Kessy amesema mabadiliko ya tabia nchi huwa hayaadhiri sehemu moja yanaadhiri sehemu mbalimbali Duniani, njia mojawapo ya kukabiliana na hali hiyo ni kuwa na njia madhubuti pamoja na mikakati ambayo kwa kushirikiana na wazalishaji hasa wakulima ambao wanafanya shughuli zao katika ardhi ambazo kwa njia moja ama nyingine zinaadhiri mazingira.
Kwa upande wake Mtafiti wa Ushiriki wa Taasisi ya Utafiti wa Mambo ya kiuchumi na Mambo ya jamii Osward Mashindano amesema mahusiano ya mabadiliko ya tabia Nchi na mambo ya vyakula ni kitu kipana kidogo lakini inahusu mabadiliko ya mazingira ya nchi kama kupotea kwa rutuba kwenye udongo kutokana na mvua kuwa zinanyesha kwa wingi kwa sehemu moja kwa muda mfupi na kusababisha mmomonyoko wa ardhi na kupoteza rutuba na kuhatarisha kilimo na kusababisha mimea kuadhirika.
"Mabadiliko ya tabia nchi yanaadhiri Sana Mikoa mingi lakini sifa iliyotufanya kuchukua Mkoa wa Tanga ni kwa kuwa Kuna sifa ya kuwa na aina zote za udongo wa hali ya hewa." Amesema Mashindano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...