Na Abdullatif Yunus - Michuzi Tv Kagera.

Kazi ya Uwekaji Taa za Barabarani Katika Manispaa ya Bukoba, imeanza rasmi katika hatua ya majaribio ya Taa hizo ambapo zoezi hilo limeanzia Eneo la Kituo cha Afya Rwamishenye Machi 26, 2022.

Itakumbukwa Kazi hii ilianza hapo awali katika hatua ya ujenzi wa Vizimba vya Kushikilia milingoti ya Taa hizo, Na mara baada ya hatua hiyo ilitakiwa kazi ya kufunga Taa kuendelea lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza na kupelekea kazi hiyo kuchelewa na sasa Shughuli hii inatekelezwa chini ya Mkandarasi MOLLEL ELECTRICAL CONTRACTORS kutoka Dar es Salaam wkishirikiana na TANROADS.

Akizungumza na Mwandishi wetu Meneja wa Mradi Mhndisi Medard J. Rweikiza amesem zoezi hilo la majaribio limenzia eneo hilo la Rwamishenye ambapo Zoezi litachukua Siku 24, lakini siku 14 zitatosha kutoa Matokeo, wakati ambapo kazi ya kufunga Taa hizo maeneo mengine itakuwa ikiendelea.

Aidha Mhandisi Medard ameongeza kuwa ucheleweshwaji wa Taa hizo kufungwa ulichagizwa na Ugonjwa wa Korona ambapo baadhi ya Mizigo ya Vifaa hivyo ilichelewa kuwasili.

Taa hizo zinafungwa ikiwa ni Ahadi ya Chama cha Mapinduzi Jimboni Bukoba Mjini ambapo Mbunge wa Jimbo hilo Stephene Lujwahuka Byabato aliahidi Manispaa ya Bukoba kuwekwa Taa za Barabarani.

Fundi wakiendelea na Shughuli ya Kufunga Soral Pane lkabla ya kusimamisha Nguzo ya Kushikilia Taa.
Soral Panel ya Watt 220 ikiwa Tayari imekwishafungwa kwenye Nguzo na Shughuli ya kufunga Taa ikiendelea.

Mhandisi Medard Rweikiza  kutoka Mollel Eletrical Contarctors ambaye ndiye Meneja Mradi akihakkikisha kila kitu kinakaa sawa.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...