Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele (kushoto) pamoja na mkuu wa kikosi namba  834 JKT Makutupora Dodoma, Luteni Kanali Festo Mbanga (kulia) wakati alipokuwa akitoa maagizo ya upandaji miti  pembezoni mwa barabara ya kuingia jiji la Dodoma leo Machi 26,2022.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewataka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi namba 834 Makutupora kilichopo mkoani Dodoma kupanda miti pembezoni mwa barabara ya kuingia jiji la Dodoma ili kuhifadhi mazingira pamoja na kupendezesha eneo hilo.

Makamu wa Rais amesema hayo alipotembelea eneo hilo la JKT Makutupora ambapo amesisitiza uwepo wa kambi hiyo ya jeshi katika eneo hilo ni kwa sababu ya ulinzi wa chanzo cha maji katika bonde la mzakwe hivyo wanapaswa kufanya uhifadhi huo kikamilifu.

Aidha Makamu wa Rais amewataka JKT Makutupora kuhakikisha wanadhibiti waharibifu wa mazingira na waoingiza mifugo na kuchoma mkaa jirani na chanzo cha maji mzakwe. Amesema serikali imeweka mkazo katika uhifadhi wa mazingira na tayari imeleekeza upandaji miti katika ngazi za kaya ambapo kila kaya inapaswa kupanda miti mitatu hadi mitano kulingana na maeneo husika.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Rajabu Mabele amesema JKT itatekeleza kikamilifu maagizo hayo na kuweka mkazo katika uhifadhi wa eneo hilo na sehemu zinginezo zinazohusika na JKT.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...