Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, amekutana na kuzungumza na wazee wa mkoa wa Arusha, na kuwahakikishia kuwa serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, itaendelea na utaratibu wa kuzungumza na wazee kila wanapowatembelea mikoa mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza mara baada ya kushiriki chakula cha jioni, Makamu wa Rais amesema kuwa mchango wa wazee katika kuliendesha taifa ni mkubwa sana, kwani wameshiriki katika kupigania uhuru wa nchi, kuhakikisha ulinzi wa wananchi na mipaka yake, usalama wa raia na mali zao lakini pia kuleta umoja na mtangamano katika nchi.
Dkt Mpango amesema kuwa tayari Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa Trilioni Moja na bilioni mia moja na hamsini kwa ajili ya kulipa wastaafiu wapatao elfu hamsini aidha amewaahakikishia kuwa serikali inaendelea kushughulikia changamoto za wazee kwa kutambua mchango mkubwa walioiletea na wanayoendelea kuiletea taifa, aidha amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya sekta ya afya, ikiwemo hospitali, kuongeza upatikanaji wa dawa, kufundisha wataalam na kununua vifaa vya kisasa.
Makamu wa Rais amewaasa wazee wa mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa wanahamasisha jamii kushiriki katika zoezi la sensa ya watu na makazi ambalo linatarajiwa kufanyika mwezi wa nane mwaka huu, amesema kuwa kupitia sensa hiyo, serikali itaweza kujipanga vyema katika kuleta maendeleo, kuwahudumia wazee, watoto na wenye mahitaji maalum. Ameongeza kuwa serikali linajadili swala la bima la afya kwa watanzania na pindi litakuwa tayari, watanzania watanufaika na huduma hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wazee wa Arusha, Mzee Selewa ameshukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuthamini mchango wa wazee katika kuleta maendeleo ya taifa, aidha ameiomba serikali kuendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili wazee zikiwemo, ulipwaji wa pensheni kwa wakati na kupata bima za afya bila urasimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, akizungumza na wazee wa mkoa wa Arusha wakati akiwa ziarani katika mkoa huo. Machi 14,2022
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, akisalimiana na wazee mbalimbali wa mkoa wa Arusha, mara baada ya kuzungumza naoi wakati akiwa ziarani mkoani humo. Machi 14,2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...