Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango akiwasili Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mtumba
Jijini Dodoma kwaajili ya kuzungumza na watumishi wa Wizara hiyo leo
tarehe 23 Machi 2022.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira, mazungumzo yaliofanyika Ofisi ya Wizara hiyo Mtumba Jijini
Dodoma leo tarehe 23 Machi 2022.
*******************
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Philip
Mpango leo tarehe 23 Machi 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na
watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, mazungumzo
yaliofanyika Ofisi ya Wizara hiyo Mtumba Jijini Dodoma.
Katika
mazungumzo hayo Makamu wa Rais alipokea changamoto mbalimbali
zinazowakabili watumishi hao pamoja mapendekezo na maoni ya watumishi ya
namna bora ya kutekeleza majukumu ya wizara hiyo yenye dhamana ya
Mazingira na Muungano hapa nchini.
Akizungumza
na watumishi hao, Makamu wa Rais amewataka kufanya kazi kwa bidii,
nidhamu pamoja na kufuata kanuni na maadili ya Utumishi wa umma wakati
wote wanapotekeleza majukumu yao. Aidha amewataka kuwa na ushirikiano na
Ofisi pamoja na Wizara zingine ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
zaidi.
Amesema
wajibu wa Wizara hiyo ni kuhakikisha inalinda na kudumisha Muungano
hivyo amewataka watumishi hao kushiriki vikao vya kamati ya pamoja vyote
kama ilivyopangwa na kutatua changamoto zinazojitokeza pamoja na
kuimarisha yale mazuri yote yanayohusu Muungano.
Ameiagiza Wizara hiyo kuhakikisha inaongeza kasi ya utoaji elimu ya
muungano kuanzia shule za msingi mpaka vyuo vikuu, kwa watumishi wa
serikali pamoja na jamii kwa ujumla.
Amesema jamii inapaswa kutambua sifa nzuri za muungano na kuitaka
wizara kutumia njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii pamoja na
Sanaa.
Halikadhalika
amewataka watumishi wa idara ya mazingira kuhakikisha wanasimamia
kikamilifu suala la mazingira ikiwemo upandaji miti pamoja na usafi wa
mazingira.
Amesema matatizo kama yaliojitokeza mto Mara hivi karibuni na
kusababisha vifo vya viumbe hai katika mto huo yanapswa kutambulika
mapema kufuatia ufuatiliaji wa karibu wa mazingira.
Amewataka
watumishi wa wizara hiyo kuwa wa mfano katika suala la upandaji miti na
kuwataka kuchukua hatua binafsi za utunzaji mazingira katika maeneo
wanayoishi.
Pia
Makamu wa Rais amewataka kuendelea kufuatilia maazimio ya kimataifa
pamoja kuongeza ushirikiano na wadau wa mazingira, sekta binafsi,
taasisi za kimataifa , dini pamoja na taasisi za fedha ili kupata
teknolojia rahisi pamoja na upatikanaji wa fedha utakaowezesha
kutekeleza program mbalimbali za mazingira.
Awali
akimkaribisha Makamu wa Rais kuzungumza na watumishi hao, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo
amesema Wizara itaendelea kuwa kioo katika suala la muungano na ajenda
ya utunzaji mazingira pamoja na na tayari mafanikio yameanza kuonekana
ikiwemo wananchi mbalimbali kuanza uuzaji na upandaji wa miti katika
maeneo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...