Mama Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli, amesema ataendeleza utamaduni waliyojiwekea yeye na marehemu mume wake wa kutoa misaada kwa wenye uhitaji wakati wa sikukuu za kidini ili kugawana na wenzao kidogo walichojaaliwa nacho.
Mama Magufuli ameyasema hayo wakati akikabidhi misaada mbalimbali kwa kwaya 100 zenye uhitaji, wafungwa, pamoja na watoto yatima katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 18, 2022.
Amesema ameamua kutoa misaada hiyo katika kipindi hiki ambapo waumini wa dini ya Kikristo duniani kote wako katika mfungo wa Kwaresima wa siku 40 ikiwa ni ishara ya kushiriki mateso pamoja na Yesu Kristo, aliyejitoa sadaka kuteswa, kufa msalabani na baada ya siku tatu akafufuka ili kumkomboa mwanadamu.
"Kipindi cha Kwaresima ni cha kufunga na kufanya toba. kutafakari maisha yetu, tujikane nafsi zetu kwa kutenda matendo mema na kujizuia kutenda vitendo viovu ili kujisogeza karibu na Mwenyezi Mungu.
"Katika kipindi hiki tunaaswa kiusaidia wenye uhitaji na shida mbalimbali kwani (Mithali 19:17) Amhurumiayte masikini humkloipesha Bwana; Naye atamlipa kwa tendo lake jema", alisema Mama Magufuli, ikiwa ni siku moja baada ya kuadhimisha kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hjayati Dkt. Magufuli iliyoongoza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mjini Chato.
Misaada alioyotoa ni pamoja na mchele tani 3.2, Maharage tani 3.4, sabuni za miche za kufulia katoni 50 pamoja na sare za wanafunzi 500, ikiwa ni za wasichana jozi 250 na idadi hiyo hiyo ya jozi kwa wavulana.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Martha Mkupasi, Mbunge wa Chato Dkt Medard Kalemani, Mkuu wa Gereza la Chato Bw. Raphael Magesa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw. Batholomew Manunga pamoja na viongozi wa dini, wadau wa maendeleo na wananchi.
Mama
Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John
Pombe Magufuli, akimsikiliza Mbunge wa Chato Dkt. Medard Kalemani,
wakati wa hafla aliyoandaa Mama Magufuli kwa kuikabidhi misaada kwa
ajili ya kwaya zenye uhitaji, wafungwa, pamoja na watoto yatima
iliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 18, 2022.
Mama
Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John
Pombe Magufuli, akimkabidhi misaada kwa wawakilishi wa kaya 100 wakati
wa hafla aliyoandaa Mama Magufuli kwa ajili ya kutoa misaada kwaya zenye
uhitaji, wafungwa, pamoja na watoto yatima iliyofanyika nyumbani kwake
Chato mkoani Geita leo Machi 18, 2022.
Mama
Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John
Pombe Magufuli, akipata picha ya kumbukumbu na watoto yatima wanaolelewa
katika vituo vya Ibn Ghanim cha Bwanga, Angel's Home cha Rulenge na
Buseresere wakati wa hafla aliyoandaa Mama Magufuli kwa ajili ya kutoa
misaada kwa kwaya zenye uhitaji, wafungwa , pamoja na watoto yatima
iliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 18, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisindikizwa na Mama Janeth Magufuli, Mjane wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Magufuli, baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la hayati Dkt. Magufuli katika siku ya kumbukizi ya mwaka mmoja ya kifo cha kiongozi huyo nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Machi 17, 2022.
Picha na Muhidin Issa Michuzi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...