Na Victor Masangu
MKURUGENZI mtendaji wa kampuni ya Ako Selina Koka katika kuwakomboa wanawake kuondokana na wimbi la umasikini ameamua kuwawezesha kiuchumi kwa kuanzisha jukwaa la uwezeshaji ambalo litaweza kuwasaidia kuondokana na changamoto zinazowakabili na kuachana na kuwa tegemezi.

Selina ambaye pia ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Silvesrty Koka aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya .mwanamke duniani ambayo yaliambata na ufunguzi rasmi wa jukwaa hilo ambalo linawajumuisha wanawake wapatao 125 ambapo ilifanyika Katika ukumbi wa urafiki Jijini Dar es Salaam.

"Katika kuunga mkono juhudi ambazo zinafanywa na Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan nimeanzisha jukwaa hili ambalo kwa sasa lina jumla ya wanawake wapatao 125 kutoka Mkoa wa Dar es Salaam na lengo lake kubwa ni kuwasaidi kujikwamua kiuchumi na kutimiza malengo yao,alisema Selina

Aidha alimpongeza kwa dhati Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mipango madhubuti ya kuwasaidia wakinamama wajasiriamali mbali mbali ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia fedha mbali mbali wanazipatiwa.

"Mwanamke ni Taifa kubwa katika jamiii ambayo itatuzunguka pamoja na familia kwa ujumla hivyo sisi tukiwezeshwa tunaweza kufanya kazi na kujitegemea wenyewe na kitu kikubwa cha msingi wanatakiwa wachape kazi kwa bidii na kutobweteka na inabidi kupeana moyo katika utekelezaji wa majukumu yetu,"aliongeza Selina

Pia alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuendelea kushirikiana bega kwa bega na wanawake wengine katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia nyanja mbali mbali na kuongeza kwa sasa wameshafungua akaunti yao ambayo wameanza na kiasi cha shilingi milioni sita.

Kwa upande wake mmoja wa wanawake aliyehudhulia katika halfa hiyo Asha Baraka amempongeza Mama Koka kwa kuanzisha jukwaa hilo la wanawake kwani litaweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kiuchumi na kufanikisha kutimiza malengo yao.

"Nampongeza Mama Koka kwa hatua hii nzuri na kipekee nimshukuru Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutuongoza vizuri katika nchi yetu pamoja na tutuwezesha sisi wakinamama wajasiriamali yeye ni Jemedali wetu,"alisema Asha.
Picha ya pamoja. 
Mkurugenzi mtendaji aa kampuni ya Ako Selina Wilson Akizungumza Jambo na waandishi wa habari hawapo pichani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...