NA BALTAZAR MASHAKA,Kahama


MWENYEKITI wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja, amesema mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan, madarakani yako mafanikio mengi Watanzania wameyaona,wameyasikia,wamejifunza na kuyafanyia tathmini ili kuyawekea mkazo.

Pia amesema jambo moja kubwa Watanzania wapaswa kuifahamu historia ya nchi zinazofuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ikiwemo Tanzania na mifumo yake halisi ya kupata viongozi,utamaduni ambao umejengeka kwa miaka mingi ili uwe mazingatio kwa sasa na siku zijazo.

Akizungumza leo mjini Kahama,kuhusiana mafanikio ya mwaka mmoja wa uongozi wa nchi yetu chini ya Rais Samia,amesema licha ya kupokea nchi kipindi cha majonzi,amefanya mambo makubwa ya maendeleo ya kupigiwa mfano yanayoonekana kwa macho ndani ya muda mfupi.

Amesema yapo mengi ya maendeleo,kiuchumi,kijamii na kisiasa yamefanyika ndani ya mwaka mmoja ambayo Watanzania wameyasikia na kuyaona ikiwemo miradi ya kimkakati wanapaswa kufanyia tathmini na kuyatilia mkazo kwa ustawi wa nchi.

“Kabla sijazungumzia uongozi shupavu uliotukuka wa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan,nianze kuwakumbusha historia za nchi zote za Kikomunisti, mfumo wake mkuu wa kupata viongozi wazuri kwanza viongozi huandaliwa kuwa viongozi wenye kuzingatia maadili ya kiutumishi na uongozi wa umma,”amesema Mgeja.

Amesema nchi za kijamaa ikiwemo Tanzania, zina mfumo rasmi wa kupata viongozi wazuri walioandaliwa kiuongozi na kutahadharisha mfumo huo wa kupata viongozi walioandaliwa ukiachwa au kuusaliti, dhambi yake lazima iwatafune waliokuwemo na wasiokuwemo,nchi kwa ujumla wake itatikisika.
Akizungumzia uongozi wa nchi,Mgeja amesema taifa lina bahati kubwa kumpata kiongozi aliyeandaliwa,Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan,ni ukweli usiopingika nchi kupata kiongozi aliyeandalika inatulia tuli kama maji ya mtungi,inabaki kuona jinsi gani ya kujiletea maendeleo kwa haraka na kuufanya mstakabali wa nchi kuwa mzuri katika nyanja za kisiasa na kiuchumi.

Mwenyekiti huyo wa taasisi hiyo inayojishughulisha na Utawala bora,Haki na Demokrasia,amedai ili kujua kiongozi ni yupi na ni wa aina gani,ni anayeonekana kuongoza kwa kushirikisha wengine,hiyo Mama Mhe. Samia ni kiongozi mzuri anayetoa uongozi na kuonyesha njia pamoja na maono yake kwa anaowaongoza.


“Mwaka mmoja wa Mhe. Rais wetu akiwa Ikulu, ameonyesha uwezo mkubwa sana na karama ya uongozi uliojaa ukomavu mkubwa wa kisiasa na maono makubwa,hekima na busara,ana upendo na wananchi wake,ni kiongozi shupavu aliyeshiba dini na hofu ya mwenyezi Mungu, anachukia dhuluma na anataka kuona haki inasimama, hayo yote ni matunda mema ya kupata kiongozi aliyeandalika,”ameeleza.

Mgeja amewakumbusha Watanzania kwa kunukuu maneno ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kuwa ili tuendelee tunahitaji mambo manne nayo ni watu,ardhi,siasa safi na uongozi bora.

“Katika uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia, falsafa hiyo ya Baba wa Taifa tunaona anavyoifanyia kazi vizuri sana,ni imani yetu tuko vizuri na tunaendelea kuwa vizuri kimaendeleo na kiuchumi,”amesema na kuongeza;


“Mh. Rais Samia chini ya uongozi wake imara na shupavu,kwa siku 365 amezidi kutufanya Watanzania wamoja bila kujali dini,ukabila, kanda, siasa na jinsia,pia kazi kubwa njema kwenye uongozi wake ameshirikisha makundi mbalimbali ya vijana, wazee,wanawake wakiwemo viongozi wa dini, wanasiasa, machifu, wafanyakazi na wakulima, wafanyabiashara na machinga, wanamichezo na wasanii.”

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, ndani ya siku hizo madarakani,wananchi wanaishi kwa matumaini makubwa yaliyojaa faraja,uhusiano wetu na mataifa mengine duniani kibiashara na kidiplomasia yamerejea na yanaendelea kukua kwa kasi kubwa na kuindoa nchi yetu katika dhana iliyotaka kujengeka kuwa ni kisiwa.

Ameeleza kuwa mwaka mmoja wa uongozi wa Rais Samia na Amiri Jeshi Mkuu, hoja 11 zinazoelezea kero za Muungano wetu zimeondolewa na kuufanya uendelee kuimarika,ulinzi na usalama umeimarika,wananchi wanaishi kwa amani na usalama wakifanya kazi na shughuli za kujiletea maendeleo.“Hii ndio agenda kubwa namba moja,kama hakuna amani maendeleo hayatakuwepo na hata wawekezaji hawawezi kuja kuwekeza nchini, niwaombe Watanzania bila kujali dini, kabila, ukanda na wanasiasa kumuombea na kumuunga mkono Mhe. Rais Samia aendelee kulitumikia Taifa la Tanzania kwa weledi na kuliletea maendeleo,naamini kufikia mwaka 2025 nchi yetu itapaa kwa maendeleo.”amesistiza mwanasiasa huyo mkongwe


Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation yenye makao yake mjini Kahama, Hamisi Mgeja akisisitiza jambo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu hatima ya uongozi na mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.Picha na Baltazar Mashaka


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...