Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa Dkt.Edmund Mndolwa akiwa mkoani Njombe ametoa wito kwa jumuiya hiyo kuboresha miundombinu ya miradi ya shule za jumuiya ili ziweze kujiendesha na kudai kuwa shule zilizoshindwa kujiendesha zimeongeza madeni ya Jumuiya.
Mndolwa amebainisha hayo wakati akiielekeza Jumuiya kuwa na mapato mbadala kwa kuwa mkoa wa Njombe umebarikiwa kuwa na hali nzuri ya hewa na kudai kuwa Jumuiya hiyo inamiliki miradi ya shule mbili ikiwemo ya Ludewa sekondari na Masimbwe sekondari.
“Niwaase kwenye hizi shule mbili mlizo nazo,shule kama haiwezi kujiendesha inaongeza madeni ya Jumuiya na ndio maana madeni yetu ya Jumuiya yameongezeka”alisema Mndolwa
Aidha amebainisha shule hizo zimekuwa zikiongeza ghalama za kila mwaka mpaka kwa Chama cha Mapinduzi.
“Shule zikituongezea ghalama ya kila mwaka pia zinakwenda kumuongezea mzigo CCM kinachotakiwa ni kufaulisha wanafunzi kwenye shule zetu
Ameongeza kuwa kutokana na shule zinazomilikiwa na Jumuiya ya wazazi kushindwa kufanya vizuri watahakikisha mabadiriko makubwa ili kuendeleza miradi hiyo.
“Takribani shule 30 hazifanyi vizuri,tutahakikisha tunajenga jina zuri la jumuiya ya wazazi na watu wakimbilie kwenye shule zetu kabla ya kwenda kwenye shule zingine na hili linawezekana.Na sasa tumetengeneza muongozo ambao bado unapita kwenye mchakato wa baraza”alisema Mndolwa
Kwa upande wake katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Njombe Bwana Sure Mwasanguti amesema shule nyingi za Jumuiya zimeshindwa pia kuendelea kuokana na kukosa ubunifu
“Hili swala la shule za wazazi hili walimu wengine sio wabunifu yaani amekaa miaka yote lakini yuko hapo hapo bila kufanya maendeleo”
Vile vile amebainisha kuwa shule ya Masimbwe ina kila aina ya mashine huku ikikosa miundombinu ya majengo pekee.
“Kama shule ya Masimbwe ina kila aina ya mashine tulichokikosa pale ni majengo tu lakini unakuta mwalimu amekwenda na ameitelekeza vile vile labda kwasababu ya mfumo unaokuja tunaamini hizi kamati za utekelezaji wataona kama ni mradi wao kwasababu tunao wazee wengi wastaa ambao walikuwa wanafundisha na kufaulisha hawana kazi tukiwachukua na kujipatia ha kaujila kidogo yapo mambo yatabadilika”alisema Mwasanguti
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa Jumuiya hiyo amesema shule mbili za Jumuiya hizo zilizopo wilayani Ludewa zinakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa wanafunzi,Masimbwe sekondari ikiwa na wanafunzi 36 huku Ludewa Sekondari ikiwa na wanafunzi 94.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa Dkt.Edmund Mndolwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa Dkt.Edmund Mndolwa akipokewa na viongozi wa CCM katika ofisi za chama hicho mkoa wa Njombe zilizopo kata ya Mji mwema halmashauri ya mji wa Njombe.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa Dkt.Edmund Mndolwa akiwasalimia baadhi ya wanachama wa CCM wa kata ya Mji mwema.Viongozi wa CCM wakiimba wimbo wa hamasa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa Dkt.Edmund Mndolwa katika ukumbi wa Deo Sanga uliopo katika ofisi za CCM mkoa wa Njombe.Baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Njombe wakimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa Dkt.Edmund Mndolwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...