Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila ametoa siku saba kwa Kampuni ya Daska Company Ltd, kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Barabara ya Byuna/Nkindwabiye/ Halawa barabara yenye urefu wa 14.9km. Thamani ya mradi/mkataba huo ni Tsh.139.993 mln.
“Tofauti na hapo mkataba uvunjwe na taratibu zifuatwe kupata kampuni nyingine.Sina na sijawahi kuwa na subira kwa wakandarasi wababaishaji. Nitoe wito Wakandarasi wote mkae mguu sawa. Nitafuta kazi zote zinazosuasua ili kubaki na wakandarasi wenye uwezo wa kutekeleza kazi kwa mujibu wa mikataba wanayosaini”.Amesema Kafulila.
Kafulila ametoa maelekezo hayo kwa Meneja wa Mkoa wa Mamlaka ya Barabara vijijini( TARURA) wakati wa ziara yake leo Machi14, 2022 wilaya ya Bariadi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...