Na. WAF - DODOMA
Waratibu
wa tiba Asili/Mbadala wa Halmashauri wametakiwa kuwaelimisha waganga wa
tiba Asili/Mbadala juu ya sheria, miiko na maadili pamoja na usafi
wakati wa utoaji wa huduma.
Hayo yamesemwa leo machi 10, 2022 na
Mkurugenzi wa tiba Dkt. Omari Ubuguyu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
siku mbili kwa Waratibu wa tiba Asili/Mbadala jijini Dodoma.
Matumizi
ya huduma za tiba Asili/Mbadala yameongezeka na zaidi ya asilimia 60
wanatumia huduma za tiba asili kabla ya kwenda kwenye huduma za kisasa.
Dkt.
Ubuguyu ameendelea kutoa wito kwa Waratibu hao kuendelea kuratibu
huduma hizo katika Halmashauri zao ikiwa ni pamoja na kukemea vitendo
viovu ambavyo ni kinyume na Sheria ya tiba Asili/Mbadala Na. 23 ya mwaka
2002 ikiwa ni pamoja na kupiga ramli chonganishi.
"Kwa pamoja
tuliona muitikio wa jamii juu ya matumizi ya dawa za tiba asili katika
kupambana dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19, huu ni uthibitisho tosha kuwa
huduma hizi zinakubalika na kuaminika na jamii". Amesema Dkt. Ubuguyu
Amewakumbusha
kuwa jukumu la waratibu ni kuhakikisha jamii inapokea huduma salama
ambayo haihatarishi Afya ya jamii na hayo yote yatawezekana kama
watasimamia shughuli za tiba Asili/Mbadala kwa weledi na nidhamu.
Kwa
upande wake Mratibu wa tiba Asili/Mbadala kutoka Morogoro Bi. Elizabeth
Kibela ameshukuru wizara ya Afya kupitia Tiba Asili/Mbadala kwa
kuanzisha mafunzo hayo.
"Mafunzo haya yataenda kutujengea uwezo
mzuri kwa kwenda kuwafundisha wanganga na kuwakumbusha juu ya kufuata
sheria, miiko na maadili ya tiba asili". Amesema Bw. Kibela
Mafunzo
hayo kwa waratibu wa tiba Asili/Mbadala yakayo fanyika kwa siku mbili
yamehusisha Mikoa minne ambayo ni pamoja na Dodoma, Morogoro, Singida na
Tabora.Mkurugenzi
wa idara ya Tiba Dkt. Omari Ubuguyu akifungua mafunzo kwa Waratibu wa
tiba Asili/Mbadala wa ngazi ya Halmashauri wa Mikoa minne ambayo ni
Dodoma, Morogoro, Singida na Tabora yatakayo fanyika kwa siku mbili
mkoani Dodoma
Afisa
kutoka Ofisi ya msajili wa tiba Asili/Mbadala Bi. Eleonorah Erio akitoa
mafunzo kwa Waratibu wa tiba Asili/Mbadala wa Halmashauri za Mikoa ya
Morogoro, Singida, Tabora walipokutana jijini Dodoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...