Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya METL Mohammed Dewji kwa kuahidi kufadhili masomo kwa madaktari wawili watakaosomea masomo ya ubingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.
Waziri Ummy ametoa pongezi hizo jana wakati wa maadhimisho ya miaka nane ya taasisi ya ufadhili wa masomo ya Mo Dewji Foundation inayodhaminiwa na mfanyabiashara huyo yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam.
Waziri Ummy amesema ufadhili wa masomo kwa Madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo utasaidia kuondokana na uhaba wa madaktari hao ambao wako 16 nchi nzima huku mahitaji ya nchi ni kuwa na madaktari kati ya 500 hadi 600.
Aidha, Waziri Ummy amesema ili kuweza kutimiza mahitaji ya nchi kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO) inatakiwa kuwa na daktari mmoja atakayetoa huduma kwa kila watu 100,000, tofauti na hali iliyopo hivi sasa ya uhaba mkubwa wa madaktari bingwa hao nchini inawafanya kuhudumia wagonjwa wengi.
"Licha ya Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kutenga Shilingi bilioni 3 kwenye bajeti ili kuwasomesha madaktari bingwa lakini nawaomba wafanyabiashara na wawekezaji kutoa ufadhili wa masomo wa kada mbalimbali za afya kwa vijana wa kitanzania ili kuweza kupata wataalam wataosaidia kukidhi mahitaji ya nchi". Amebainisha Waziri Ummy.
Taasisi ya MO Dewji kupitia Mo Scholars Program imetoa ufadhili kwa wanafunzi wa kitanzania zaidi ya 120 katika fani mbalimbali kwenye Vyuo Vikuu vya University of Dodoma (UDOM), University of Dar es salaam (UDSM), Mzumbe University, Sokoine University of Agriculture (SUA), Mbeya University of Science and Technoloy, Centre for Foreign Relations, Dar es Salaam Institute of Technology, College of Business Administration (CBE), pamoja na Institute of Finance Management na State University of Zanzibar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...