Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Mpango kabambe wa kuhakikisha uzalishaji wa chakula katika kongani ya kilombero inayoshughulika na kuendeleza kilimo mkoa wa Morogoro chini ya Kituo cha kuendeleza kilimo nyanda za kusini mwa Tanzania (SAGCOT) umejadiliwa kuhakikisha uzalishaji wa mazao unaongezeka ili kuihakikishia nchi usalama wa chakula.

Akizungumza kwenye kikao cha siku mbili kilichoandaliwa na Ofisi ya Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na SAGCOT na wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo uliofanyika jana mjini Morogoro, Mkuu wa Mkoa huo Bw.Martine Shigela amekipongeza kituo cha SAGCOT kwa kazi nzuri wanayofanya na kuitaka kuendelea kufanya kazi na Ofisi yake kwa karibu ili kuleta tija katika uzalishaji na kuifanya morogoro kuwa kitovu cha uzalishajI mazao hapa nchini.

"Nipende kuipongeza SAGCOT kwa namna inavyojitoa kuhakikisha yule mkulima mdogo ananufaika kwa kufanya kilimo chenye tija kwa kumpatia elimu juu ya kilimo biashara, sambamba na kumkutanisha na wadau katika mnyororo mzima wa thamani katika Sekta ya kilimo." Alisema Bw. Shigela

Alisema Safari hiyo ya kilimo waliyoianza haitoishia hapo itakuwa na muendelezo wa vikao ambavyo zitakavyoleta mrejesho wa utekelezaji kwa yaliyopendekezwa na zaidi kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazomkabili mkulima mdogo ili kuongeza hali ya uzalishaji mazao hususani katika kongani ya kilombero.

"Huu ni mwanzo tunategemea kuwa na vikao vingine ambavyo vitawakutanisha wadau wengi zaidi, wakiwemo wenyeviti wa vyama wilaya na Mkoa, viongozi wa vyama vya ushirika, viongozi wa wakulima, wazalishaji, wasindikaji, taasisi za kifedha na wanunuzi wa mazao.’’Alisema Bw.Shigela

Aliongezea kuwa Morogoro kijiografia inaardhi nzuri kwa kilimo cha mazao mbalimbali na pia inaendana na mikoa mbalimbali hivyo kwa kuongeza uzalishaji wa mazao kutapelekea mkoa kupiga hatua kiuchumi na kimaendeleo kupitia sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Bw. Geoffrey Kirenga amesema kikao hicho cha siku mbili kimehusisha wadau mbalimbali kutoka Sekta binafsi na Umma ambao mwisho wa kikao watakuja na mbinu za kuhakikisha uzalishaji wa chakula unaongezeka nchini.

"Lengo la kikao hiki ni kuona kilimo kinatoa mchango mkubwa kwa taifa sambamba na kumuinua mkulima mdogo kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji kwa kufanya kilimo endelevu ambacho ni rafiki kwa mazingira." Alisema Bw. Kirenga

Alisema Serikali kwa kishirikiana na wabia wa maendeleo wamefanya kazi kubwa katika kukuza na kuendeleza Sekta ya kilimo nakuongeza kuwa wakati umefika kwa wakazi wa mkoa wa Morogoro kuchangamkia fulsa ya kuwekeza kwenye kilimo.

"Mkoa wa Morogoro ni mkoa uliobarikiwa kuwa na eneo lenye ardhi kubwa, njema na nzuri ambayo inakubali mazao mengi hivyo nitoe rai kwa wakazi wa Morogoro kuanza kuwekeza kwenye kilimo kwani kitawatoa katika dimbwi la umaskini."Alisema Bw. Kirenga.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo(ASA), Dkt. Sophia Kashenge alisema kikao hiko kimeonyesha malengo mazuri katika kuendeleza kilimo nchini hivyo wao kama wakala wa mbegu wamejipanga vyema kuhakikisha wanazalisha mbegu zenye ubora ili kuleta tija katika uzalishaji wa mazao nchini kama sehemu ya maazimio ya kikao hiko.

"Tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunazalisha mbegu nyingi zenye ubora ambao zitamletea matokea chanya mkulima, kwani matokeo mazuri katika uzalishaji yaanzia katika ubora wa mbegu, "alisema Dkt. kashenge

Kikao hicho cha siku mbili kimeratibiwa na SAGCOT kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kuwakutanisha wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo pamoja na taasisi binanfsi.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Martine Shigela (katikati) akizungumza kwenye kikao cha kwenye  kikao cha siku mbili kilicholenga kujadili changamoto na namna ya kukuza uzalishaji mazao katika kongani ya Kilombero  kilichoandaliwa  na Ofisi  ya Mkoa huo kwa kushirikiana na  Kituo cha kuendeleza kilimo nyanda za juu kusini mwa Tanzania(SAGCOTna kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya Umma na Sekta Binafsi jana mjini Morogoro. Kushoto ni  Katibu  Tawala  wa Mkoa wa Morogoro Bi.  Mariam Mtunguja na wapili kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Bw. Geoffrey Kirenga na kulia ni  kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Muslimu.


 
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Martine Shigela (kulia) akiteta jambo na  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Bw. Geoffrey Kirenga (kushoto)  kwenye  kikao cha siku mbili kilicholenga kujadili changamoto na namna ya kukuza uzalishaji mazao katika kongani ya Kilombero  kilichoandaliwa  na Ofisi  ya Mkoa huo kwa kushirikiana na  SAGCOT  na kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya Umma na Sekta Binafsi jana mjini Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...