Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha March 23
WAKAZI
 wa kata ya Pangani , Kibaha Mjini Mkoani Pwani pamoja na Diwani wa kata
 hiyo Agustino Mdachi wameeleza Hali mbaya ya upatikanaji huduma ya maji
 safi na salama ,kwakuwa wanataabika kutumia maji ya visimani,mtoni 
,kwenye madimbwi ama kununua dumu na ndoo kwa sh.500.
Hali
 hiyo imewapa taabu kwa kipindi kirefu kwani licha ya Kuwa katika Mji wa
 Mjini yaani Kibaha Lakini ni kata iliyokuwa inakosa huduma ya maji.
Hayo
 yalibainika ,wakati baadhi ya wajumbe kamati ya siasa CCM mkoa na 
kamati ya siasa mji wa Kibaha ,iliposhiriki ukagua ujenzi wa mradi wa 
kituo cha afya Kidimu na mradi wa tenki la maji Vikawe, kata ya Pangani 
utakaojumuisha ujenzi wa matenki makubwa ya ujazo wa lita milioni tano 
pamoja na usambazaji kwa watumiaji tenki la Vikawe ikiwa ni sehemu ya 
mradi huo wa matenki matatu.
Diwani
 wa kata ya Pangani, Mdachi alisema ,kwasasa Wana matumaini ya 
kuondokana na kero hiyo baada ya mradi wa tenki la maji Vikawe, 
kukamilika kwa asilimia zaidi ya 90.
"Hali
 Ni mbaya ,kwani Halmashauri ya Mji wa Kibaha changamoto kubwa ya maji 
ipo kata ya Pangani ,Ila Hali ya mradi inatumainisha upo kwenye asilimia
 zaidi ya 90 na tumeelezwa ifikapo mwezi wa sita mwaka huu kero hii 
itabaki historia."
"Serikali
 imetambua uhitaji wetu ,Tunashukuru Sana ,nimekuwa nisali usiku na 
mchana moja ya changamoto za kata hii ziishe ili nami Kama diwani niweze
 kusema Jambo katika utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM"
Akizungumzia
 ujenzi wa kituo cha afya Kidimu ,Mdachi alisema kata hiyo ilikuwa haina
 kituo cha afya, wakazi wa kata hiyo wanafuata huduma za afya umbali 
mrefu kituo cha afya Mkoani na hospital ya rufaa ya mkoa Tumbi.
Alisema, ujenzi ulipofikia asilimia 50 pia wanatarajia kuondokana na adha ya kufuata huduma za kiafya umbali mrefu.
Mkazi wa Kidimu ,kata ya Pangani ,Bahati Omar alieleza wana matumaini kwa Sasa baada ya kuona ujenzi unakamilika wa maji .
"Tulikuwa
 tunatoka majumbani unakwenda kuchimba vijisima ili kupata maji ,uwezo 
wetu wengine sisi Ni wa Hali ya chini hatumudu sh .500 kwa ndoo ,unajua 
matumizi ya nyumbani ndoo kwa siku ziwe japo tano hapo kupikia, matumizi
 ya chakula ,usafi ,watoto ,baba yaani hayatoshi ,na huwezi kununua maji
 bila chakula ,kiukweli Ni Hali mbaya "
Bahati
 alisema kwamba, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa milioni 250 kukamilika 
ujenzi wa kituo hiki Cha afya Kidimu kupitia fedha za tozo ,wanashukuru 
kwakuwa Ni mkombozi kwa afya za watoto na wanawake ambao kwa kiasi 
kikubwa wanapata shida.
Mhandisi
 kutoka DAWASA Kibaha,Fred Mushi alieleza ,awamu ya kwanza mradi 
utalisha mitaa vya Vikawe Shule, Vikawe Bondeni Kidimu Miwalebaada ya 
hapo wakikabidhi dawasa itafikisha mitaa mingine ikiwemo mtaa wa 
Mkombozi.
"Hatua iliyopo Ni usukumaji maji na tunatarajia ujenzi kukamilika June 2022"alifafanua Mhandisi Fred.
Mwenyekiti wa CCM Pwani ,Ramadhani Maneno CCM imetoa maelekezo mikoa ipitie miradi kisha ipeleke taarifa kwa mkuu wa mkoa.
"Mimi
 na wenzangu mkoa tumejigawa ,tumepitia miradi ,tumeridhishwa na 
utekelezaji Lakini nasisitiza miradi iendane na thamani ya fedha 
"Mh.Rais ametoa fedha hizi zitumike kwa malengwa sahihi "alieleza 
Maneno.
Kwa upande wake 
Mwenyekiti wa CCM Kibaha Mjini, Maulid Bundala alielekeza mradi wa 
ujenzi wa kituo cha afya ikamilike mwezi ujao ili itoe huduma haraka na 
mhandisi wa DAWASA wakamilishe mradi Kama walivyoahidi June 16 mwaka 
huu.
Mkurugenzi wa 
Halmashauri mji Kibaha, Mshamu Munde alisema wanasimamia miradi 
kikamilifu na wataalamu wa Halmashauri wanaendelea kufanya majukumu yao 
ili kuhakikisha inaleta tija kwa wananchi.


 


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...