Kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imefanya ziara ya kutembelea na
kukagua mradi wa maji wa Kigamboni (Kisarawe II ) ili kujionea Maendeleo
ya mradi huo ikiwa ni mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassani.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na
Maji, Mhe. Dkt.Christina Ishengoma amesema anamshukuru Rais Samia
Suluhu Hassan kwa kuweza kutenga pesa kwenye mradi wa maji wa Kisarawe
II ili kuondoa hadha ya upatikanaji wa maji katika eneo la Kigamboni
pamoja na maeneo ya pembezoni.
Pia
ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kwa
kuweza kusimamia na kutekeleza miradi huo maji kikamilifu.
"Kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji tumeyapokea taarifa ya mradi wa
Kisarawe II na pia tumetembelea ili kujiridhisha na kuona kuwa hakuna
tatizo la kutaa mradi wa maji kwani wa DAWASA kwani kazi inaonekana"
alisema Dkt. Ishengoma
Naye
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa shukrani
kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuongeza bajeti ya mwaka
2021/2022 kwenye Wizara ya Maji ili kuhakikisha wananchi wa Dar es
Salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla wanapata majisafi na Salama ikiwa
na lengo la kumtua mama ndoo kichwani.
"Mamlaka
za maji nchini zinatekeleza miradi kama hii ya DAWASA ili kuweza
kuondokana na tatizo la maji katika Mikoa yote hapa nchini" alisema
Mahundi
Naye
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi wa
Maji Kisarawe II unahusisha uendelezaji wa visima kumi na mbili vya maji
vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 57 pamoja na ujenzi wa tanki la kuhufadhia maji litakaloweza kuhifadhi maji lita Milioni 15.
“Mradi
huu unatekelezwa kwa sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ujenzi wa kituo
cha kusukuma maji, kituo cha kupokea Maji, ulazaji wa mabomba ya maji na
ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhi maji la lita milioni kumi na tano
linalojengwa Kigamboni na awamu ya pili ikihusisha kazi ya kufunga njia
za umeme kwenye visima na kutoa maji kwenye visima na kupeleka kwenye
kituo cha kusukuma maji amesema Luhemeja.
Luhemeja
amesema Mradi huu ulianza kutekelezwa mwezi Disemba mwaka 2019 huku
ukigharimu kiasi cha bilioni 24 fedha za ndani za Mamlaka na kukamilika
kwakwe kutanufaisha wakazi 250,000 wa maeneo ya Kibada, Mjimwema,
Masonga, Kimbiji, Mpera na maeneo ya karibu.
Kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati
hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhe.
Mhandisi Maryprisca Mahundi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi
Cyprian Luhemeja kuhusu moja ya kisima chenye urefu mita 600 kwenda
chini kilichopo katika kata ya Kisarawe II katika Wilaya ya Kigamboni
wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji
ilipotembelea mradi huo Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati
hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhe.
Mhandisi Maryprisca Mahundi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi
Cyprian Luhemeja kuhusu namna mabomba ya maji yatakavyolazwa mara baada
ya kumalizika kwa ujenzi wa tanki la kuhufadhia maji linalojengwa
Kigamboni wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji
ilipotembelea mradi huo Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati
hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhe.
Mhandisi Maryprisca Mahundi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi
Cyprian Luhemeja kuhusu akipokea taarifa kuhusu mradi wa maji wa
Kigamboni(Kisarawe II) utakavyoweza kuhudumia kata 7 za Kigamboni wakati
wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea
mradi huo Kigamboni mkoani Dar es Salaam
Kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati
hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhe.
Mhandisi Maryprisca Mahundi wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya aMajisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi
Cyprian Luhemeja kuhusu ujenzi wa tanki la kuhufadhia maji litakaloweza kuhifadhi maji lita Milioni 15 linalojengwa
Kigamboni wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji
ilipotembelea mradi huo Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati
hiyo Mhe. Dkt.Christina Ishengoma pamoja na Naibu Waziri wa Maji, Mhe.
Mhandisi Maryprisca Mahundi wakitembelea Mradi wa ujenzi wa Tanki la
kuhifadhia maji wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji
ilipotembelea mradi huo Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Ziara ikiendelea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...