Aliyeonyesha nia wa Kugombea kiti cha Urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na Mwanaharakati wa maendeleo ya watu, dkt.Maryrose Majinge amewataka watanzania kujifunza kuyatazama mambo mema yanayofanywa na viongozi na kuacha dhana na fikra mbaya kwa watu hao.
Amesema, watu walikuwa wakidhani kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan hataweza kuongoza nchi kwa kuwa ni mara ya kwanza kwa nchi kuongozwa na mwanamke lakini katika kipindi hiki cha mwaka mmoja amedhihirishia Wananchi na mataifa yote kuwa anaweza.
Amesema kuwa watu waliokuwa wanamtazamo juu juu kuwa Rais Samia hataweza fikra zao hasi hazinamuafaka mwema kwa taifa. "Tumekuwa tukimfikiria vibaya mama tukisema tusubiri tuone huyu hawezi,huku ni kujichulia ubaya ile ni taasisi anaweza"
Ameeleza kuwa mwaka mmoja wa Rais Samia umetoa taswira ya tumeona kwa mwaka mmoja alivyofanya mambo mazuri basi wenye mashaka tusimame kuona kuwa mama anaweza" amesema Dk Marryrose.
Dk. Majinge amependekeza sheria ya Mvuto kutumika vizuri ili kuondosha tabia ya kudhaniana mambo yasiyopendeza (mabaya) tabia ya kuamini mtu fulani hawezi inaturudisha nyuma.
"Tunakuwa mbali na mtu fulan kwa sababu unamuona hafai lakini tunapaswa kujua kila mtu ana upungufu wake na uimara wake , ndio maana wabobezi wa masuala ya maelendeleo ya watu wanasisitiza sheria ya mvuto, ili mtu atende mambo mazuri lazima umtabirie mambo mazuri kwake kama moyoni mwako unadhana mbaya kila alitendalo mtu huyo hutaliona zuri" amesema DK Majinge.
Ameitaja Sheria ya mvuto kuwa inakusudia watu wawaze mambo mazuri, kanuni ya dhahabu inataka umpendelee mwenzako yale tunayoyapenda wewe.
Ameeleza kuwa sheria hiyo ya Mvuto ikitumiwa sambamba na kanuni ya dhahabu watu wataondokana na fikra hasi kutilia mashaka kuogopana.
Pia amesema kuwa kanuni ya kuwa na matumani yaani watu kutokataa tamaa itaboresha fikra za watu.
Amesisitiza kuwa watu kuacha tabia ya kuyatazama mambo kwenye upande wa ubaya "Tabaia iliyojengeka ni kutazama udhaifu au ubaya nasi kutazama upande wa mazuri"

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...