Na Andrew Chale, Chalinze.

Mbunge Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amekagua ujenzi wa shule ya Sekondari inayojengwa katika Kijiji cha Msolwa huku akiwataka wazazi kuhimiza watoto wa kike kupatiwa elimu ilikuwa na akina Mama Samia wajao.

Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hayo leo Machi 7, 2O22 wakati wa kukagua ujenzi wa shule ya Sekondari inayojengwa katika Kijiji hicho eneo la Makondo mengi

Ambapo amesema: "Mafanikio ya ujenzi wa Shule hii ya Sekondari Msolwa yanakwenda kuwezesha kuwapo kwa Wakinamama Samia wengi siku zijazo" alisema Mh. Kikwete

Na kuongeza kuwa, Serikali inafanya juhudi kuhakikisha wanasogeza huduma muhimu ikiwemo hiyo ya shule ambapo itakuwa mkombozi kutokana na watoto wanaofaulu kwenda mbali kufuata shule za sekondari.

"Tunashukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Shilingi Milioni 600 zilizowezesha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Msolwa," Alisema.

Ujenzi wa shule hiyo utapunguza kero ya wanafunzi kufuata huduma hiyo mbali kwani wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali wakiwemo watoto wa kike.

"Kazi Inaendelea Chalinze ili kuendana na kasi ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutaka Kazi Iendelee" alimalizia Mhe. Ridhiwani.

Ujenzi huo naoendelea unatarajia kukamilika mwakani huku ikitarajiwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Msolwa na Vijiji jirani
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...