Na Fredy Mshiu
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji imeridhishwa na usimamizi na utekelezaji wa miradi ya Maji ya Kibamba-Kisarawe na Pugu-Gongo la mboto iliyotekelezwa na DAWASA kwa kupitia fedha za ndani.

Akiongea wakati wa ziara ya kamati hiyo kwenye miradi ya maji Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Mhe. Jerry Silaa (Mb) amesema hali ya usambazaji maji katika Jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani inaridhisha hususani katika maeneo yaliyokuwa sugu na upatikanaji wa Maji kama vile Kisarawe na Pugu.
"Mfano mzuri ni hapa tulipo katika jimbo la Ukonga, ambapo kwa takribani miaka 40 hapakuwepo huduma ya majisafi, lakini utekelezaji wa mradi wa Pugu-Gongo la mboto umemaliza changamoto hiyo iliyodumu kwa muda mrefu".ameleeza Mh.Slaa

Mheshimiwa Slaa ameongeza kuwa kwa kasi wanayoenda nayo DAWASA kamati inaamini ifikapo 2025 itakuwa imewafikia Wananchi wote katika eneo lake la kihuduma.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja ameeleza kuwa kazi kubwa imefanyika na inaendelea kufanyika, katika usambazaji wa maji ili kuhakikisha yanawafikia wananchi wote.
"Tulipokea Maelezo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Samia Suluhu Hassan kuharakisha usambazaji wa maji kwa wananchi katika maeneo ambayo miradi imekamilika. Lakini pia tumepokea maelekezo ya Kamati katika kuharakisha usambazaji wa huduma ya maji na tunaenda kutekeleza hilo kwa kasi".ameeleza Mhandisi Luhemeja.

Ndugu Bakari Utingo, mkazi wa Kata ya Majohe ameishukuru DAWASA kwa kufikisha huduma ya maji katika kata zote za Pugu na kwa sasa maji ni Mengi na ya uhakika.
"Nakumbuka Mara ya mwisho maji kutoka bombani katika kata yetu ya Majihe ni mwaka 1999, tumekuwa tukitumia maji ya visima na kununua kwa watoa huduma binafsi kwa muda mrefu. Tunashukuru sasa tumefikishiwa huduma na DAWASAna niwaombe waendelee na kasi ya kuunganisha huduma ya maji kwa wananchi wengi zaidi".ameeleza Utingo

DAWASA inatekeleza miradi mikubwa na midogo mbalimbali ili kufikia asilimia 95 ya upatikanaji ifikapo 2025.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...