Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amemuelezea hayati Magufuli kuwa ni miongoni mwa viongozi bora waliowahi kutokea Barani Afrika kwa namna alivyokuwa mtu mwema, mbunifu na mwenye moyo wa kulijenga taifa lake kwa upendo na kwa usawa.
Mhe. Spika ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Magufuli, yaliyofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita leo machi 17, 2022.
Aidha, Mhe. Dkt. Tulia amemshukuru na kumpongeza Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuyaendeleza mambo mazuri ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoanzishwa na hayati Magufuli kitendo alichokieleza kuwa ni kuwafuta machozi ya watanzania walio wengi.
“Mheshimiwa Rais, siku ya leo ni siku ya kukumbuka mtangulizi wako alipoiaga dunia lakini tunafurahi kwamba kumbukizi hii haiji na majonzi tena bali inakuja na ushindi mkubwa ambao Mheshimiwa Rais umetufikisha hapa kwa kuyafanya mambo makubwa yakiwemo yale ambayo unayaendeleza kutoka kwa mtangulizi wako na zaidi yale ambayo unayafanya kwa utashi wako.” Amesisitiza Spika. Dkt. Tulia.
Maadhimisho hayo yaliyoongozwa na Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, yamehudhuriwa pia na Viongozi mbalimbali wa serikali, dini na wananchi mbalimbali kutoka maeneo tofauti nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...