Na Amiri Kilagalila,Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe mteule Waziri W.Kindamba amepokewa na baadhi ya watumishi wa mkoa huo pamoja na kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo mhandisi Marwa Rubirya aliyestaafu kwa umri.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba amefika mkoani Njombe na kukabidhiwa ofisi ikiwa ni siku moja imepita tangu alipoapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan hapo jana Ikulu jijini Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba akikabidhiwa ua kama ishara ya upendo na ukaribisho mkoani Njombe wakati akipokewa na baadhi ya watumishi wa mkoa wa Njombe nje ya ofisi za mkoa huo.Kushoto ni aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya akimkabidhi baadhi ya taarifa za mkoa huo mkuu wa mkoa mpya wa Njombe Waziri Kindamba wa kulia mara wakati wa kukabidhiwa ofisi hiyo
Mkuu wa mkoa mpya wa Njombe Waziri Kindamba akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika ofisi ya mkoa wa Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...