Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima ametaka wazazi kutoa kupaumbele katika kusomesha watoto wa kike tangu wakiwa wadogo ili kuzalisha kizazi cha viongozi bora wanawake.

Aidha, ametoa wito kwa taasisi na mashirika mbalimbali kuwapa kipaumbele wanawake wenye sifa za kuwa viongozi katika taasisi hizo.

Malima amesema hayo leo Jumanne Machi 8, katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

"Mkoa wa Tanga umebarikiwa kwa kuwa na viongozi wengi wanawake na hivi tunavyozungumza tuna wabunge wanne wanawake mkoani kwetu na wanaupiga mwingi mno huko bungeni. Hii inapatikana kwa kusomesha watoto wa kike.

"Si wabunge tu tuna wakuu wa wilaya watatu wanawawake, wakuu wa idara nyeti za serikali karibu wote wanawake na dunia sasa hivi inatutambua kama mfano wa uongozi bora kupitia kwa mama yetu kipenzi Rais Samia Suluhu Hassan.

"Lakini pia wanawake ni waaminifu, ukitaka kuthibitisha hili angalia takwimu katika mikopo ya vikundi inayotolewa na halmashauri, wanaorejesha wengi ni wanawake kwa asilimia 65 kulinganisha na vijana na walemavu, mimi naona wanawake waongezewe mikopo," amesema Malima.

Pamoja na mambo mengine, Malima amewataka watu wote wanaokutana na ukatili wa kijinsia kutoa taarifa ili hatua zichukuliwe.

"Ikiwa kazini mtu anakunyanyasa kutokana na jinsia yako, usikae kimya. Natoa wito kwa asasi zinazotoa elimu ya masuala ya kijinsia kujitokeza kutoa elimu ya kijinsia mkoani Tanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...