Na Mwandishi Wetu.

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ridhiwani Kikwete amewahakikishia Watanzania kuwa Serikali imejipanga kutatua migogoro ya ardhi ikiwemo ile ya mipaka ya Wakulima na wafugaji.

Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hayo mapema Machi 15,2022 wakati akishiriki uzinduzi wa Wiki ya Maji Simanjiro Mkoani Manyara ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.

Akitoa salamu za Wizara ya Ardhi, Mhe Ridhiwani Kikwete amempongeza na kumshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga bajeti itakayowezesha utekelezaji wa majukumu ikiwemo kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji, mipaka baina ya Wilaya, Mikoa na Hifadhi na Usalama wa Ardhi.

"Wizara ya Ardhi imejipanga kuleta amani na utulivu kwa kutatua changamoto kwenye mipaka ya ardhi." Alisema Mhe. Ridhiwani Kikwete.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...