Viongozi mbali mbali wakimsikiliza kwa makini Mhandisi Peter Ulanga akitoa mafunzo kuhusu uchumi wa kidijitali kwenye ukumbi wa mikutano wa Marijani Hoteli uliopo eneo la Pwani ya Mchangani, Zanzibar baada ya kufunguliwa na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Hussein Katanga (aliyeketi meza kuu kushoto) akiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Hussein Katanga (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (aliyeketi wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi wa tatu kulia) na viongozi wanawake baada ya ufunguzi wa mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi hao kuhusu uchumi wa kidijitali yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Marijani Hoteli uliopo eneo la Pwani ya Mchangani, Zanzibar
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (wa tatu kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Hussein Katanga wakati wa mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi wa Serikali kuhusu uchumi wa kidijitali yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Marijani Hoteli iliyopo eneo la Pwani ya Mchangani, Zanzibar. Anayesikiliza katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt. Jabiri Bakari Kuwe (wa kwanza kushoto)
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Hussein Katanga (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (aliyeketi wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi wa tatu kulia) baada ya ufunguzi wa mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi hao kuhusu uchumi wa kidijitali yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Marijani Hoteli uliopo eneo la Pwani ya Mchangani, Zanzibar
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza wakati wa mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi kuhusu uchumi wa kidijitali yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Marijani Hoteli iliyopo eneo la Pwani Mchangani, Zanzibar. Aliyeketi akisikiliza ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Hussein Katanga.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akizungumza na viongozi mbali mbali wakati wa mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi hao kuhusu uchumi wa kidijitali yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Marijani Hoteli iliyopo eneo la Pwani Mchangani, Zanzibar.
Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Hussein Katanga akifungua mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi kuhusu uchumi wa kidijitali kwenye ukumbi wa mikutano wa Marijani Hotel iliyopo eneo la Pwani ya Mchangani, Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...