Na Jane Edward, Arusha

Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo Tanzania (TEMDO)imewekeza zaidi ya shilingi Bilioni 3 kwaajili ya kukabiliana na changamoto ya vifaa tiba nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari  Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko TEMDO Sigisbert Mmasi,wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)

Amesema kuwa tayari wamesha tengeneza aina Saba za vifaa tiba kati ya vifaa tiba kumi na Saba ambavyo wanatarajia kuvitengeneza ili kukabiliana na changamoto ya uagizwaji wa vifaa hivyo nje ya nchi.

"Hapa Tanzania wadau ambao wanatengeneza vifaa vya kitabibu ni wachache na sisi kama taasisi ya kiserikali tumeona tuanze kutumia wabunifu wetu katika kutengeneza vifaa tiba ili kupunguza gharama za kuagiza nje "Alisema Mmasi

Aidha Dokta Mmasi ameiomba Serikali kuelekeza taasisi zake za afya kununua vifaa tiba kutoka taasisi hiyo ya TEMDO kwa gharama nafuu na kuacha kulipa fedha za kigeni katika kuagiza vifaa hivyo.

Nao baadhi ya wadau wa afya James Lomnyaki anasema kuwa wazo la taasisi hiyo litasaidia kupungua kwa gharama za usafiri ambapo walikuwa wanaagiza vifaa kwa kutumia fedha za kigeni na sasa TEMDO wanaona kama mkombozi.

Amebainisha kuwa kwa upande wa serikali  pia utawasaidia kupunguza gharama kubwa ya uagizaji na fedha hizo zitatumika katika utekelezaji wa shughuli zingine za kimaendeleo.

Hata hivyo taasisi hiyo pia inajihusisha na kutengeneza mashine za aina mbalimbali kama vile mashine za kutengeneza siagi ya karanga , unga lishe, mtambo wa kukamua na kusafisha mafuta ya alizeti.

Profesa Frederick Kahimba Mkurugenzi Temdo akionesha mitambo iliyobuniwa na taasisi hiyo.
Wadau wa teknolojia wakisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa TEMDO.

Dkt Sigisbert Mmasi akionyesha moja ya mitambo iliyopo katika taasisi ya TEMDO.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...