Na Mwandishi Wetu, Geita
TAASISI inayohusika na michezo kwa Walemavu wa akili Tanzania 'Special Olympics Tanzania imetoa wito kwa jamii kuendelea kuwapa kipaumbele watoto wenye ulemavu wa akili pamoja na kuwashirikisha kwenye nyanja ya michezo.
Akizungumza hivi karibuni katika mafunzo ya siku mbili yaliyofanyika mkoani Geita katika shule ya sekondari Wasichana ya Nyankumbu ikishirikisha washiriki wakiwa ni walimu 10 wa shule za msingi maalum na 10 za wasio walemavu, Mkurugenzi wa Specila Olympics Tanzania, Charles Rays alisema idadi kubwa ya wazazi wenye watoto walemavu kutowaficha ndani na badala yake wanatakiwa kuwashirikisha kwenye masuala ya maendeleo.
Rays alisema mafunzo hayo yamefanikishwa na mradi wa Stavros Niarchos Foundation (SNF) wenye dhima ya kuleta ukaribu wa kujifunza na kucheza kwa watoto wenye ulemavu wa akili na wasio na ulemavu wa akili mashuleni, lengo likiwa ni kuleta ushirikishi kwa walemavu wa akili katika jamii na kuondoa unyanyapaa
Mkurugenzi huyo ambaye ndiye alikuwa mkufunzi wa mafunzo hayo, alibainisha kuwa katika mradi wa SNF kwa awamu ya pili wamelenga kuzifikia shule 30 katika mkoa wa Geita na Kigoma, huku shule hizo zikipatiwa vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo mipira 3 ya soka, mipira miwili ya Volleyball, bips 20 pamoja na net Moja ya volleyball kwa kila shule shiriki.
Walimu ambao wameshiriki katika mafunzo hayo ni walimu kutoka shule ya msingi Nyanza, Kasamwa, Mrisho ,Nyakato, Buhalahala, Mgusu, Nyankumbu, Mbugani, Geita, Mwatulole zote za mkoani geita.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Ofisa Elimu wa mkoa wa Geita, Anton Mtweve ambaye alitumia fursa hiyo kuishukuru Special Olympics Tanzania na kueleza kuwa Geita ipo tayari katika kuhakikisha wanafunzi wenye ulemavu wa akili wanapata fursa sawa katika kila nyaja ili kuleta usawa kwa jamii.
Katika hatua nyingine Mtweve amewataka walimu waliopata mafunzo ya michezo jumuishi kuwa chachu katika jamii ikiwemo kuwasaidia walimu wengine kuwaelewesha katika kile ambacho wameelekezwa kwenye mafunzo hayo na kuwahakikishia kuwa ofisi yake ipo bega kwa bega na walimu hao.
Mkurugenzi wa Special Olympichs Tanzania, Charles Rays (kulia), Ofisa Elimu Mkoa wa Geita Anton Mtweve wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule za walemavu na wasio walemavu mkoani humoMkurugenzi wa Special Olympics Tanzania, Charles Rays akitoa mafunzo kwa walimu wa shule mbalimbali mkoani Geita, mafunzo yaliyofanyika kwa siku mbili hivi karibuni (
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...