Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba, amewasihi wataalamu wa masomo mbalimbali ya ufundi kutoka katika shule za Sekondari, Vyuo vya Ufundi na Vyuo Vikuu kuweka umakini katika mapitio ya vitabu vinavyotarajiwa kuanza kutumika shuleni mara baada ya uandaaji wake kukamilika.

Dkt. Komba ameyasema hayo leo tarehe 27/03/2022 katika kikaokazi na watalamu hao cha mapitio ya vitabu 34 vya kiada vya masomo ya ufundi kwa shule za sekondari za ufundi kilichofanyika mjini Morogoro ambapo amesema,kuwa vitabu hivyo vinatarajiwa kumsaidia mwanafunzi wa Kitanzania katika kupata ujuzi utakaopelekea kujiari ama kujiarika hivyo wanapaswa kuifanya kazi hiyo ya mapitio kwa weledi.

“Nina imani kazi hii ya kufanya mapitio mnaifanya kwa uangalifu mkubwa na kwa weledi ili lengo kusudiwa litimie”, amesema Dkt Komba.

Kazi ya mapitio imefanyika kuanzia tarehe 24 hadi 30 Machi 2022 Mjini Morogoro katika Chuo cha Ualimu

Mwezi Juni 2021, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (DIT) ziliingia makubaliano ya uandishi wa vitabu hivyo ambavyo vitaanza kutumika shuleni hivi karibuni.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...